Sunnah ya Raatibah inamtosha mtu kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid II

Swali: Nikiingia msikitini kabla ya Dhuhr na nataka kuswali Raatibah inayokuwa kabla ya Dhuhr ambayo ni Rak´ah nne. Je, kwanza nianze kuswali Tahiyyat-ul-Masjid kisha ndio niswali Rak´ah nne au Tahiyyat-ul-Masjid inaingia ndani ya zile Rak´ah nne [za Raatibah]?

Jibu: Tahiyyat-ul-Masjid inaingia ndani ya zile Rak´ah nne. Kwa msemo mwingine ukiswali Raatibah kunakutosheleza kutohitajia kuswali Tahiyyat-ul-Masjid. Ni kama ambavyo iwapo ndio unaingia msikitini ukamkuta imamu anaswali swalah ya faradhi na ukajiunga pamoja naye kunakutosheleza kutohitajia kuswali Tahiyyat-ul-Masjid. Kwa sababu malengo ya hizo Rak´ah mbili za mamkuzi ni kwamba mtu asiketi chini mpaka kwanza aswali Rak´ah mbili. Ni mamoja Rak´ah hizo mbili ni Naafilah, Raatibah au za faradhi.

Lakini ametaja kuswali Rak´ah nne kama swalah ya Dhuhr. Inatakiwa itambulike kuwa Rak´ah nne hizi zinaswaliwa kwa salamu mbili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=ydjTd-4u4ec
  • Imechapishwa: 13/06/2019