Sunnah wa namna kaburi la maiti linavyotakiwa kuwa

Swali: Je, unaweza kutubainishia sifa ya kumzika maiti? Je, inajuzu kumzika katika nyakati zote?

Jibu: Sunnah katika kumzika maiti ni kuchimbiwa mwanandani upande wa magharibi wa kaburi lake na kuwekwa humo akiwa ameshakafiniwa na kufunikwa, hata uso hautakiwi kufunuliwa; awe amefunikwa wote ndani ya mwanandani. Kisha huwekewa matofali ya kushikana juu ya mwanandani ili kufunga sehemu zote kusiingie udongo, kisha humwagiwa udongo juu yake. Baada ya hapo udongo hupanda juu kiasi cha upana wa futi moja ili ijulikane kwamba ni kaburi. Hiyo ndiyo Sunnah katika maziko.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31694/ما-صفة-الدفن-الشرعي-للميت
  • Imechapishwa: 14/11/2025