Sunnah ni kufunga mikono wakati wa kuswali

Swali: Kuna makinzano kati ya wanazuoni katika kufunga na kuachia mikono. Ni lipi sahihi zaidi kwa njia ya Qur-aan na Sunnah?

Jibu: Kilichothibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kupitia Hadiyth ya Waail bin Hujr na Sahl bin Sa´d (Radhiya Allaahu ´anh) ni kufunga mikono. Ni kuweka kiganja cha kuliani juu ya kiganja cha kushotoni juu ya kifua.  Bora ni kuiweka juu ya kifua. Ambaye ataachia mikono swalah yake ni sahihi lakini ameacha kitendo ambacho ni sahihi zaidi. Haitakikani ndugu kuvutana juu ya jambo hili. Bali wanatakiwa kukumbushana kwa hekima na kwa njia nzuri kwa ajili ya kutafuta faida. Nimeandika juu ya masuala haya kijitabu kifupi.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/146)
  • Imechapishwa: 24/10/2021