Swali: Ni lazima kwa mwanamke anapokuwa msikitini kati ya wanawake na anaswali nyuma ya imamu afunike uso wake?

Jibu: Halazimiki kufanya hivo akiwa kati ya wanawake na mbele yake hakuna wanaume wa kando naye. Katika hali hiyo Sunnah ni yeye kuacha uso wazi. Lakini asionyeshe kitu katika nywele zake. Anapasa kufunika nywele, kichwa na mwili wake mzima mbali na uso. Lakini kama anaswali mbele ya wanamme basi anatakiwa kufunika uso wake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (20)
  • Imechapishwa: 16/07/2021