Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:
160 – an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema:
واللهِ لَتُقِيمُنَّ صفوفَكم أو ليُخالِفَنَّ اللهُ بينَ قلوبِكم
“Ninaapa kuwa mtazipanga safu zenu au Allaah atatia uadui kwenye mioyo yenu.”[1]
Katika Hadiyth hii kuna dalili juu ya uwajibu wa kufanya safu zikawa sawa. Ni wajibu kwa maamuma kuzinyoosha safu zao. Wasipofanya hivo basi wameziweka nafsi zao wenyewe katika adhabu ya Allaah. Kauli hii, nikiwa na maana ya kunyoosha safu, ndio sahihi.
Ni wajibu kwa maimamu wazitazame safu. Wakiona upenyo, kuna aliyesogea mbele au kurudi nyuma, wamzindue mtu huyo. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wakati mwingine alikuwa akipita kati ya safu na kuziweka sawa kwa mkono wake mtukufu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), akianzia safu ya kwanza mpaka ya mwisho.
Pindi watu walipozidi kuwa wengi katika zama za makhaliyfah ´Umar bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´ann) akawa anamwamrisha mtu afanye safu ziwe sawa pale kunapokimiwa swalah. Anapokuja na kusema zimeshapangwa sawa ndio anakabiri kuanza kuswali. Hali kadhalika ndivo alivofanya ´Uthmaan (Radhiya Allaahu ´anh). Alikuwa amewakilisha mtu aziweke sawa safu za watu. Anapokuja na kusema zimeshawekwa sawa ndio anakabiri kuanza swalah. Hili linaonesha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na makhaliyfah waongofu walikuwa wakitilia umuhimu suala la kunyoosha safu.
Kwa masikitiko makubwa maimamu wa leo wanapuuza suala la kunyoosha safu. Wakuta mtu ametangulia na mwingine yuko kwa nyuma, lakini hata hivyo hajali.
[1] al-Bukhaariy na Muslim
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/289)
- Imechapishwa: 11/12/2024

Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/289)
Imechapishwa: 11/12/2024
https://firqatunnajia.com/sunnah-iliyosahauliwa-na-maimamu-wengi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)