Swali: Je, katika Sunnah ya Raatibah inayo sujuud ya kusahau?

Jibu: Sujuud ya kusahau inakuwa katika swalah ya kujitolea na swalah ya faradhi. Sujuud ya kusahau inakuwa katika swalah ya faradhi na swalah ya kujitolea. Ikiwa mtu atasahau katika swalah inayopendeza; kusahau kunakowajibisha kusujudu inakuwa kama katika swalah ya faradhi. Mfano akipata shaka kama amesujudu mara mbili au moja, atafanya sijda ya pili kisha alete sujudu ya kusahau. Akisimama kuswali Rak´ah mbili kisha akapata shaka kama ameswali Rak´ah ya pili au hapana, basi ataswali Rak´ah hiyo ya pili kisha atasujudu sijda ya kusahau.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/30984/ما-حكم-سجود-السهو-في-السنة-الراتبة
  • Imechapishwa: 19/09/2025