Swali: Kuna mwanamke anasoma Qur-aan kichwa wazi na amepitia Aayah iliyo na sujuud. Je, asujudu akiwa kichwa wazi au afunike kichwa?

Jibu: Hakuna neno kusoma kwake Qur-aan hali ya kuwa kichwa wazi. Kufunika kichwa kunakuwa ndani ya swalah. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Allaah haikubali swalah ya mwanamke anayepata hedhi isipokuwa kwa Khimaar.”[1]

Kuhusu kusujudu kwake kwa ajili ya kisomo, wale wanazuoni wenye kuona kuwa sujuud ya kisomo ni swalah basi atalazimika kufunika kichwa chake wakati anapotaka kusujudu. Wale ambao hawaoni kuwa sujuud ya kisomo ni swalah basi hatolazimika kufanya hivo. Lakini salama na tahadhari zaidi ni yeye kufunika kichwa chake wakati anaposujudu ili atoke nje ya makinzano ya wale wenye kuonelea kuwa ni lazima.

[1] Abu Daawuud (01/85) na at-Tirmidhiy (377) ambaye amesema:

“Hadiyth ni nzuri kwa tamko linalosema:

“Swalah ya mwanamke anayepata hedhi haikubaliwi isipokuwa kwa Khimaar.”

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.mufti.af.org.sa/ar/content/حكم-سجود-التلاوة-للمرأة-الكاشفة-عن-رأسها
  • Imechapishwa: 12/06/2022