Sujuud ya kisomo unaposikiliza Qur-aan kwenye kifaa cha rekodi

Swali: Ikiwa mtu anasikiliza kisomo cha Qur-aan kupitia kifaa cha kilichorekodi na msomaji akapitia Aayah ilio na sijda ya kisomo. Je, asujudu?

Jibu: Haikusuniwa kwa msikilizaji kusujudu isipokuwa anaposujudu msomaji. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alisomewa Suurah “an-Najm” na Zayd bin Thaabit na hakusujudu na yeye Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusujudu. Hiyo ikafahamisha kuwa Sujuud ya kisomo sio lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakumkemea Zayd kule kuacha kwake.

Hadiyth inafahamisha pia kwamba msikilizaji hatosujudu isipokuwa pale ataposujudu msomaji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/415)
  • Imechapishwa: 14/11/2021