Sujuud ya kisomo nje ya swalah pamoja na msomaji

Swali: Kuhusu sujudu ya kisomo nje ya swalah wakati tunaposoma Qur-aan tukiwa kundi – je, tunatakiwa kuwa na imamu tusujudu nyuma yake au inajuzu kwetu kuinuka kabla yake?

Jibu: Imamu ni yule msomaji. Akisujudu basi nanyi sujuduni nyuma yake. Asiposujudu nanyi msisujudu. Kwa sababu Zayd bin Thaabit (Radhiya Allaahu ´anh) alimsomea Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) Suurah “an-Najm”, Zayd wala Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuna yeyote aliyesujudu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (54) http://binothaimeen.net/content/1239
  • Imechapishwa: 19/09/2019