Siwaak mbele za watu


Swali: Ni ipi hukumu ya kutumia Siwaak mbele za watu? Baadhi ya watu wanasema ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haswali isipokuwa nyumbani kwake. Kwa hivyo wanasema kuwa haipendezi mtu akaswali mbele za watu. Je, haya ni sahihi?

Jibu: Mosi ni kwamba yale aliyomnasibishia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni uwongo. Hadiyth isemayo:

”Alikuwa anapoingia nyumbani kwake anatumia Siwaak.”[1]

ndani yake haikusema kuwa alikuwa anaswaki nyumbani pekee.

Pili zipo Hadiyth nyingi zinazokokoteza kuswaki wakati wa kila swalah na wakati wa swalah ya mkusanyiko. Haya hufanyika mbele za watu. Zipo Hadiyth nyinginezo zinazojulisha kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameamrisha Siwaak mpaka ikakhofiwa meno yake yasije kung´oka[2]. Hii ni dalili kuswaki kwa wingi.

Kubwa linaloweza kusemwa ni kwamba kuswaki mbele za watu kunaweza kupelekea mtu kujionyesha. Lakini mtu asimuhukumu mwenzake kwa jambo hilo. Ni jambo liko mikononi mwa Mola wa walimwengu.

[1] Muslim (02/15).

[2] Ameipokea at-Twabaraaniy na baba yangu ameisahihisha kupitia Hadiyth nyinginezo. Tazama ”as-Swahiyhah” (1556).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sa-altu Abiy, uk. 109-110
  • Imechapishwa: 01/07/2022