Siwaak ina dawa yake maalum?

Swali: Baadhi ya madaktari wametengeneza dawa ya meno wakasema imetengenezwa kutokana na msingi wa mti wa salvadora persica. Je, unachukua nafasi ya Siwaak?

Jibu: Hapana, dawa ya meno inahitaji gharama, inahitaji maandalizi. Lakini Siwaak haina gharama wala maandalizi. Isipokuwa kama dawa ya meno inahitajika katika baadhi ya nyakati kwa ajili ya kusafisha mdomo katika muda mwingine tofauti na wakati wa swalah, basi hilo halina shida. Lakini wakati wa swalah Sunnah ni kutumia Siwaak pekee.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28501/هل-المعجون-المصنوع-من-السواك-يقوم-مقامه
  • Imechapishwa: 21/04/2025