Swali: Je, imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tafuteni msaada katika kutimiza haja zenu kwa kuzificha?”
Jibu: Hapana, hilo si Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Linapokewa kuwa ni katika maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh).
Swali: Je, hili[1] linahusu siri kwa ujumla?
Jibu: Ni kuhusu siri ambazo kufichuliwa kwake kunaleta madhara na kunakhofiwa kwamba mwenye siri hataridhia kufichuliwa kwake, ni mamoja iwe ni kuhusu kujamiiana au jambo jingine.
Swali: Je, mwanamke anaruhusiwa kumwambia mama yake au dada yake?
Jibu: Hafai kufichua siri, si kwa mama yake wala kwa dada yake, hata kwa baba yake.
Swali: Ikiwa mwanamke huyu amepewa talaka na mwanaume, kisha mwanaume huyo anataka kumuoa mwanamke mwingine na mwanamke huyu anaogopa kwamba dada yake anaweza kudhurika?
Jibu: Siri haifichuliwi isipokuwa mwenye siri akiruhusu au sababu iliyokuwa inalazimisha kufichwa kwake iondoke.
[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Miongoni mwa watu waovu zaidi siku ya Qiyaamah ni mwanamume anayekaribiana na mke wake na mke anamkaribia, kisha anasambaza siri yake.” (Muslim)
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/2555/232-من-باب-حفظ-السر
- Imechapishwa: 11/03/2026
Swali: Je, imesihi kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Tafuteni msaada katika kutimiza haja zenu kwa kuzificha?”
Jibu: Hapana, hilo si Hadiyth ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Linapokewa kuwa ni katika maneno ya ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh).
Swali: Je, hili[1] linahusu siri kwa ujumla?
Jibu: Ni kuhusu siri ambazo kufichuliwa kwake kunaleta madhara na kunakhofiwa kwamba mwenye siri hataridhia kufichuliwa kwake, ni mamoja iwe ni kuhusu kujamiiana au jambo jingine.
Swali: Je, mwanamke anaruhusiwa kumwambia mama yake au dada yake?
Jibu: Hafai kufichua siri, si kwa mama yake wala kwa dada yake, hata kwa baba yake.
Swali: Ikiwa mwanamke huyu amepewa talaka na mwanaume, kisha mwanaume huyo anataka kumuoa mwanamke mwingine na mwanamke huyu anaogopa kwamba dada yake anaweza kudhurika?
Jibu: Siri haifichuliwi isipokuwa mwenye siri akiruhusu au sababu iliyokuwa inalazimisha kufichwa kwake iondoke.
[1] Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Miongoni mwa watu waovu zaidi siku ya Qiyaamah ni mwanamume anayekaribiana na mke wake na mke anamkaribia, kisha anasambaza siri yake.” (Muslim)
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/audios/2555/232-من-باب-حفظ-السر
Imechapishwa: 11/03/2026
https://firqatunnajia.com/siri-za-wanandoa-haambiwi-hata-mzazi/