Swali: Ni ipi hukumu ya maamuma kusoma al-Faatihah nyuma ya imamu?

Jibu: Wakati imamu anaposoma kwa sauti nyamaza. Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

وَإِذَا قُرِئَ الْقُرْآنُ فَاسْتَمِعُوا لَهُ وَأَنصِتُوا لَعَلَّكُمْ تُرْحَمُونَ

“Na inaposomwa Qur-aan, basi isikilizeni kwa makini na mkae kimya [mzingatie] mpate kurehemewa.” (07:204)

Swalah ikiwa ni ya kusoma kwa siri, kama Dhuhr na ´Aswr, ni wajibu kusoma al-Faatihah na kilicho sahali baada yake. Sio sawa kusoma pindi imamu anaposoma. Soma al-Faatihah wakati imamu amekaa kimya. Na ikiwa huwezi kufanya hivo haikuwajibikii kwako.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tahid-25-07-1435-01.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017