Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuacha swalah moja ya faradhi kwa makusudi?
Jibu: Anazingatiwa ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna kati ya mja na ukafiri na shirki isipokuwa kuacha swalah.”[1]
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا
“Wakafuata baada yao waovu walipoteza swalah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu Motoni.”[3]
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
“Wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.”[4]
Kwa msemo mwingine ni kwamba wasipofanya mambo hayo sio ndugu zetu katika dini. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema tena:
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
“Ole wao waswaliji, ambao wanapuuza swalah zao.”[5]
Baadhi ya Salaf wamesema:
“Tunamuhimidi Allaah ambaye hakusema wale adhabu kali kwa wale ambao wanapuuza ndani ya swalah zao.”
Kwa hivyo kuacha swalah ni ukafiri. Ni lazima kwa mtu huyo kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] Muslim (82).
[2] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
[3] 19:59-60
[4] 9:11
[5] 107:4-5
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 321-322
- Imechapishwa: 28/04/2025
Swali: Ni ipi hukumu kwa mwenye kuacha swalah moja ya faradhi kwa makusudi?
Jibu: Anazingatiwa ni kafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Hakuna kati ya mja na ukafiri na shirki isipokuwa kuacha swalah.”[1]
“Ahadi iliopo kati yetu sisi na wao ni swalah. Hivyo basi, yule mwenye kuiacha amekufuru.”[2]
Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:
فَخَلَفَ مِن بَعْدِهِمْ خَلْفٌ أَضَاعُوا الصَّلَاةَ وَاتَّبَعُوا الشَّهَوَاتِ ۖ فَسَوْفَ يَلْقَوْنَ غَيًّا
“Wakafuata baada yao waovu walipoteza swalah na wakafuata matamanio; basi watakutana na adhabu Motoni.”[3]
فَإِن تَابُوا وَأَقَامُوا الصَّلَاةَ وَآتَوُا الزَّكَاةَ فَإِخْوَانُكُمْ فِي الدِّينِ
“Wakitubu na wakasimamisha swalah na wakatoa zakaah, basi ni ndugu zenu katika dini.”[4]
Kwa msemo mwingine ni kwamba wasipofanya mambo hayo sio ndugu zetu katika dini. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema tena:
فَوَيْلٌ لِّلْمُصَلِّينَ الَّذِينَ هُمْ عَن صَلَاتِهِمْ سَاهُونَ
“Ole wao waswaliji, ambao wanapuuza swalah zao.”[5]
Baadhi ya Salaf wamesema:
“Tunamuhimidi Allaah ambaye hakusema wale adhabu kali kwa wale ambao wanapuuza ndani ya swalah zao.”
Kwa hivyo kuacha swalah ni ukafiri. Ni lazima kwa mtu huyo kutubu kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala).
[1] Muslim (82).
[2] at-Tirmidhiy (2621), an-Nasaa’iy (463) na Ibn Maajah (1079). Swahiyh kwa mujibu wa al-Albaaniy.
[3] 19:59-60
[4] 9:11
[5] 107:4-5
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 321-322
Imechapishwa: 28/04/2025
https://firqatunnajia.com/sio-ndugu-zetu/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket