Kuhusu Jamaa´at-ut-Tabliygh, hawaamrishi mema na wala hawakemei maovu wala mambo ya shirki. Ni wenye kujichanga. Mtu hawezi kumuhukumu kila mmoja katika wao. Pengine akawepo Sunniy katika wao asiyetambua mfumo au hatambui mfumo wa Jamaa´at-ut-Tabliygh na kwa ajili hiyo anakuwa ni mwenye kupewa udhuru kwa jambo hilo. Hata hivyo mfumo wao sio wa mfumo wa Ahl-us-Sunnah. Yule anayefanyia kazi mfumo wao sio katika Ahl-us-Sunnah. Kusingeulizwa baadhi ya maswali juu ya vitabu, basi tungeliwataja na kubainisha ubovu wa mfumo wao.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 389
  • Imechapishwa: 23/06/2025