Swali: Je, haipaswi kuoanisha kati ya mapokezi yanayosema kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiingia ndani ya swalah ya Fajr wakati wa giza na kwamba alikuwa akirefusha kisomo hadi kunamulika?

Jibu: Hivyo ndivyo alivyofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Alikuwa akiswali Fajr katika giza na kurefusha kisomo. Kwa sababu hiyo Abu Barzah amesema:

“Walikuwa wakimaliza swalah wakati mtu anaweza kumtambua aliyekaa karibu naye.”

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27027/صفة-صلاة-النبي-عليه-الصلاة-والسلام-للفجر
  • Imechapishwa: 21/03/2025