Swali: Ni sifa zepi kuu ambazo anatakiwa kuwa nazo mlinganizi ili aweze kulingania kwa Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?
Jibu: 1- Elimu. Ni lazima kwa mlinganizi awe na elimu na yakini:
قُلْ هَـٰذِهِ سَبِيلِي أَدْعُو إِلَى اللَّـهِ ۚ عَلَىٰ بَصِيرَةٍ
“Sema: “Hii ndio njia yangu nalingania kwa Allaah juu ya baswiyrah.” (12:108)
Bi maana kwa elimu.
2- Ikhlaasw. Anatakiwa amtakasie Allaah nia wakati wa kulingania kwake. Asiwe ni mwenye kutaka kuonekana, kusikika wala manufaa ya kidunia. Malengo yake awe ni mwenye kutaka uso na radhi za Allaah (Subhaanah). Vilevile lengo lake iwe kuwanufaisha watu.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Haqiyqatu Da´wat-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab http://alfawzan.af.org.sa/ar/node/17206
- Imechapishwa: 01/01/2018
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)