Si kwamba inajuzu, bali ni wajibu kuomba talaka!

Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuomba kujivua katika ndoa kutoka kwa mume wake ikiwa anapuuzia swalah kwa kuzikusanya zote katika wakati mmoja, hafungu na wala haswali pamoja na kwamba nimemnasihi sana ila haitikii.

Jibu: Si kwamba inajuzu, bali ni wajibu kwake kuomba kutengana naye. Ni wajibu kwake kuomba watengane na wala asibaki kwa mwanaume ambaye haswali na wala hafungi na tunaomba kinga kutoka kwa Allaah.

Check Also

Kutengana na mwanaume asiyeswali

Swali: Dada huyu anauliza anasema. Mume wangu haswali kamwe [baki ya swali haliko wazi]… Jibu: Ikiwa …