Nilimuuliza Ahmad kuhusu mtu mwenye kula na kunywa Ramadhaan. Akasema: ”Hakuna juu yake kafara.” Nikasema: ”Ni kwa nini humjalii ni kama yule ambaye amejamiiana na mkewe?” Nikasema: ”Mi nisimjaalie hivo?” Hakuna Hadiyth yoyote inayotaja hilo. Ni vipi nitamuwajibishia kafara kwa kula na kunywa ilihali Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amemuwajibishia kafara kwa kufanya jimaa? Ijapo yote hayo yanazingatiwa kuwa ni maasi, lakini kula na kunywa hakufananishwi na jimaa. Jimaa mtu anaweza kupigwa mawe na kuwajibika kuoga josho kubwa. Hakuna chochote katika hayo kinachofanana na kula na kunywa.”

  • Muhusika: Imaam Ishaaq bin Mansuur al-Kawsaj al-Marwaziy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Masaa-il-ul-Imaam Ahmad bin Hanbal wa Ishaaq bin Raahuuyah (670)
  • Imechapishwa: 01/03/2025