Swali: Inajuzu kwa mtu kumwambia ambaye amemfanyia wema na anataka kumshukuru:

“Shukurani za dhati.”?

Jibu: Mshukuru kwa kiasi cha wema:

وَوَصَّيْنَا الْإِنسَانَ بِوَالِدَيْهِ حَمَلَتْهُ أُمُّهُ وَهْنًا عَلَىٰ وَهْنٍ وَفِصَالُهُ فِي عَامَيْنِ أَنِ اشْكُرْ لِي وَلِوَالِدَيْكَ إِلَيَّ الْمَصِيرُ

“Tumemuusia mwanadamu [kuwatendea wema] wazazi wake wawili; mama yake ameibeba mimba yake akimzidishia udhaifu juu ya udhaifu na [kumnyonyesha na] kuacha kwake ziwa katika miaka mwili ya kwamba: unishukuru Mimi na wazazi wako; Kwangu ndio marejeo ya mwisho.” (23:14)

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hamshukuru Allaah yule asiyewashukuru watu.”

Mshukuru kiasi cha wema wake.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Duruus-ul-Haram http://www.alfawzan.af.org.sa/node/13382
  • Imechapishwa: 24/06/2020