Shiy´iy wa kweli anaona kuwa Abu Bakr na ´Umar ndio bora kuliko ´Aliy

Kulisemwa kuambiwa Shariyk bin ´Abdillaah bin Nimr:

“Ni nani bora kati ya Abu Bakr na ´Aliy?”

Akajibu:

“Abu Bakr.”

Akaambiwa:

“Unasema hivo ilihali wewe ni Shiy´iy?”

Akajibu:

“Shiy´ah ndiye mwenye kusema hivo. Ninaapa kwa Allaah kwamba ´Aliy alipanda juu ya mimbari na akasema:

“Watu bora katika Ummah baada ya Mitume wake ni Abu Bakr na ´Umar.”

Je, tumrudie? Je, tumkadhibishe? Ninaapa kwa Allaah kwamba hakuwa mwongo.”

Haya yametajwa na al-Qaadhwiy ´Abdul-Jabbaar katika “Tathbiyt-un-Nubuwwah” na akakiegemeza kwa Abul-Qaasim al-Balkhiy ambaye amekitunga kwa ajili ya kujibu radd ya ar-Rawandiy kwa al-Jaahidhw.

Wasomi na wachaji hawa wamepokea kwamba Abu Bakr ndiye alikuwa bora sembuse kama yeye ndiye alikuwa na haki zaidi ya kuwa khaliyfah wa kwanza. Vipi basi mtu anaweza kusema kwamba wale waliokula kiapo cha usikivu kwake walikuwa wanatafuta mambo ya kidunia au walikuwa wajinga? Uhakika wa mambo ni kwamba sifa hizi ako nazo yule mwenye kutuhumu. Kwa ajili hiyo hutowapata wowote wanaojinasibisha na Uislamu ambao ni wajinga wa kupitiliza na wenye tamaa zaidi ya dunia kama walivyo Raafidhwah.

Nimezingatia hali yote na nikapata kwamba hakuna kasoro yoyote wanayowatuhumu kwayo Maswahabah isipokuwa wao ndio watu wakubwa zaidi wenye kusifika nayo na wakati huohuo Maswahabah ndio watu walio mwisho kabisa kuhusiana na kasoro hiyo.

Hapana shaka kwamba wao ni waongo wakubwa kabisa. Mfano wao ni kama Musaylamah al-Kadhdhaab ambaye alisema:

“Mimi ndiye Mtume wa kweli na Muhammad ndio mwongo.”

Kwa ajili hii ndio maana wanajisifu wao wenyewe kwamba ndio waumini na kwamba Maswahabah ni wanafiki. Ukweli wa mambo hakuna kundi lolote ambalo ni wanafiki wakubwa kama Raafidhwah na hakuna aliye na imani kubwa kama Maswahabah.

  • Mhusika: Shaykh-ul-Islam Ahmad bin Taymiyyah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Minhaaj-us-Sunnah an-Nabawiyyah (2/86-87)
  • Imechapishwa: 23/12/2018