Swali: Sherehe ya tohara. Baadhi ya watu wamezoea kufanya tohara siku ya kuzaliwa kwa Mtume mtukufu na huchinja wanyama, huwaalika familia kadhaa na baada ya tohara humpa mtoto fedha. Je, kuna namna maalum ya kusherehekea tohara?

Jibu: Mosi ni kwamba tohara ni miongoni mwa Sunnah za kimaumbile ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alizielekeza.

Pini ni kwamba hakuna sherehe ya tohara katika Uislamu. Kufanya tohara siku ya kuzaliwa kwa Mtume pamoja na kusherehekea siku hiyo ni Bid´ah iliyozuliwa. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Yeyote mwenye kuzua katika jambo letu hili jambo ambalo halimo, basi ni lenye kurudishwa.”

Ameipokea al-Bukhaariy na Muslim.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/114)
  • Imechapishwa: 21/10/2026