Kuna baadhi ya watu wakiambiwa kitu fulani ni Sunnah wanasema “Mwanachuoni fulani amesema kadhaa na kadhaa.” Hawa ni katika wale wenye kufuata kichwa mchunga na washabiki. Kuhusiana na mwenye kutumia hoja kauli ya mwanachuoni fulani na yeye hajui kuhusu Sunnah [ya Mtume], huyu halaumiwi. Taqliyd ya mtu asiyejijua inajuzu na ni sawa.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/284)
  • Imechapishwa: 27/09/2024