Swali: Vipi hali ya watu hawa na je inatakiwa kusikiliza kanda zao; Ibraahiym ad-Duwaysh, ´Aaidh al-Qarniy, Salmaan al-´Awdah na Muhammad al-Mukhtaar ash-Shanqiytwiy?
Jibu: Nijualo kuhusu watu hawa ni kwamba hawafuati njia yetu na Da´wah yetu. Ibraahiym ad-Duwaysh, ´Aaidh al-Qarniy, Salmaan al-´Awdah na Muhammad al-Mukhtaar ash-Shanqiytwiy ni katika vigogo wa al-Ikhwaan al-Muslimuun. Tumesikia kuwa ash-Shanqiytwiy pia anafuata njia moja kama wao, hata kama atakuwa ni khafifu kuliko wao. Hawa ni katika viongozi na khaswa Salmaan al-´Awdah, ad-Duwaysh na al-Qarniy. Kadhalika ash-Shanqiytwiy ambaye analingania katika Da´wah yao na ana Taswawwuf na baadhi ya ukhuurafi.
Kwa ajili hii sisi tunawanasihi kutosheka na vitabu na kanda za Ahl-us-Sunnah. Kuna kheri ambayo – in shaa Allaah – iliosafi. Na khaswa wanachuoni waliobobea katika elimu. Hii ndio nasaha ya Ahl-us-Sunnah. Baadhi yao wamepiga mfano; ni jambo linaloingia akilini wewe uko na chanzo cha maji masafi kabisa na badala yake unakunywa kutoka kwenye chanzo cha maji machafu? Hali kadhalika inaweza kusemwa kuhusu kanda na vitabu vya Ahl-us-Sunnah. Humo kuna bayana, kheri na mawaidha yote wakati uko na uhakika na Dini yako na Manhaj yako. Tofauti na kanda za watu hawa. Watu wengi wanadai kuwa ndani yake wanaguswa kwenye nyoyo zao, mawaidha na baadhi ya faida. Hata kama unapata kitu katika faida, unaweza kuathirika kwa madhara mengine pasina wewe kujua. Mtu akiwasikiliza sana moyo unaambatana nao. Shaytwaan anampambia yale wanayokuja nayo. Ukisikiliza kaseti hizi kuhusu kuhifadhi swalah na kanda ya pili kuhusu kuwatendea wema wazazi na kanda ya tatu kuhusu Tawhiyd na kanda ya nne kuhusu kujiepusha na madhambi na maasi, moyo utaambatana na muongeaji huu. Kisha baadaye watie sumu zao katika kanda zao na vitabu vyao. Ni Ahl-us-Sunnah wangapi wamepotea kwa sababu ya kusikiliza watu hawa. Mtu anadhoofika siku baada ya siku na anaanza kuona kuwa hawa wako juu ya msitari, wapigana Jihaad na kadhaa na kadhaa. Hakuna kitu kama kuwa na moyo uliosalimika.
Kitu ninachowanasihi watu wote ni kutosheka na kusikiliza kaseti za Ahl-us-Sunnah ambao wanaaminika kwa elimu na Manhaj yao na khaswa wanachuoni waliobobea katika elimu. Utapata mawaidha yanayoongelea Kasema Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na faida za kielimu na zenye faida na kunufaika na Manhaj ya wazi kabisa, salama na ilionyooka. Tunatahadharisha ndugu zetu kusikiliza au kusoma katika vitabu vya watu hawa. Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) Anasema katika Kitabu Chake Kitukufu:
وَإِذَا رَأَيْتَ الَّذِينَ يَخُوضُونَ فِي آيَاتِنَا فَأَعْرِضْ عَنْهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ وَإِمَّا يُنسِيَنَّكَ الشَّيْطَانُ فَلَا تَقْعُدْ بَعْدَ الذِّكْرَىٰ مَعَ الْقَوْمِ الظَّالِمِينَ
”Unapowaona wale wanaoziingilia na kuzishambulia Aayah Zetu, basi jitenge nao mpaka waingie kwenye mazungumzo mengineyo. Na kama shaytwaan akikusahaulisha, basi baada ya kukumbuka usikae pamoja na watu madhalimu.” (6:68)
وَقَدْ نَزَّلَ عَلَيْكُمْ فِي الْكِتَابِ أَنْ إِذَا سَمِعْتُمْ آيَاتِ اللَّـهِ يُكْفَرُ بِهَا وَيُسْتَهْزَأُ بِهَا فَلَا تَقْعُدُوا مَعَهُمْ حَتَّىٰ يَخُوضُوا فِي حَدِيثٍ غَيْرِهِ ۚ إِنَّكُمْ إِذًا مِّثْلُهُمْ
”Naye amekwishakuteremshieni katika Kitabu kwamba mnaposikia Aayah za Allaah zinakanushwa na zinafanyiwa istihzai, basi msikae pamoja nao mpaka waingie katika mazungumzo mengineyo. Vinginevyo mtakuwa kama wao.” (4:140)
- Mhusika: Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin ´Umar al-´Adaniy
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1932&PageN
- Imechapishwa: 28/07/2020

Mhusika: Shaykh ´Abdur-Rahmaan bin ´Umar al-´Adaniy
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: http://www.olamayemen.net/Default_ar.aspx?ID=1932&PageN
Imechapishwa: 28/07/2020
https://firqatunnajia.com/shaykh-al-adaniy-kuhusu-ad-duwaysh-al-qarniy-al-awdah-na-ash-shanqiytwiy/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)