Swali: Unasemaje juu ya zakaah ambayo watu wanaitoa kwa serikali wakati wa Ramadhaan?
Jibu: Zakaah ambayo, nayo akikusudia Zakaat-ul-Fitwr, serikali wanaichukua kwa njia ya pesa. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi ya tende au pishi ya shayiri ni lazima kwa mvulana, msichana, mdogo, mkubwa, muungwana na mtumwa wa Kiislamu. Aliamrishwa itolewe kabla watu hawajatoka kuswali.”[1]
Ikimuwezekani kutoa moja katika vitu hivi vinne ni vizuri. Isipomuwezekania basi atoe kile chakula kinacholiwa sana katika mji. Kuhusu kutoa pesa, Hanafiyyah wanaona kuwa inafaa. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema pishi au thamani yake. Maoni sahihi ni kwamba pesa haitoshelezi. Hata hivyo serikali ikikulazimika kufanya hivo na wasifuate dalili, ikiwa mtu atatoa kibaba ikiwa ana uwezo wa kufanya hivo na atawapa serikali pesa ili asalimike na shari zao. Ikiwa hana uwezo wa kutoa zakaah mara ya pili basi itamtosha ile ya kwanza na dhambi zitakuwa juu ya serikali.
[1] al-Bukhaariy (1503).
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 294-295
- Imechapishwa: 04/08/2025
Swali: Unasemaje juu ya zakaah ambayo watu wanaitoa kwa serikali wakati wa Ramadhaan?
Jibu: Zakaah ambayo, nayo akikusudia Zakaat-ul-Fitwr, serikali wanaichukua kwa njia ya pesa. Abu Sa´iyd al-Khudriy (Radhiya Allaahu ´anh) amesimulia kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifaradhisha Zakaat-ul-Fitwr pishi ya tende au pishi ya shayiri ni lazima kwa mvulana, msichana, mdogo, mkubwa, muungwana na mtumwa wa Kiislamu. Aliamrishwa itolewe kabla watu hawajatoka kuswali.”[1]
Ikimuwezekani kutoa moja katika vitu hivi vinne ni vizuri. Isipomuwezekania basi atoe kile chakula kinacholiwa sana katika mji. Kuhusu kutoa pesa, Hanafiyyah wanaona kuwa inafaa. Lakini Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakusema pishi au thamani yake. Maoni sahihi ni kwamba pesa haitoshelezi. Hata hivyo serikali ikikulazimika kufanya hivo na wasifuate dalili, ikiwa mtu atatoa kibaba ikiwa ana uwezo wa kufanya hivo na atawapa serikali pesa ili asalimike na shari zao. Ikiwa hana uwezo wa kutoa zakaah mara ya pili basi itamtosha ile ya kwanza na dhambi zitakuwa juu ya serikali.
[1] al-Bukhaariy (1503).
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 294-295
Imechapishwa: 04/08/2025
https://firqatunnajia.com/serikali-inapolazimisha-wananchi-wake-kutoa-zakaat-ul-fitwr-pesa/