Sentesi zote baada ya adhaana ni Bid´ah

Swali: Baadhi ya waadhini wana ada ya kusema kwa sauti ya juu baada ya adhaana:

“Ee Allaah! Msifu na mpe amani Mtume na bwana wetu Muhammad!”

au:

الصلاة الصلاة يرحمكم الله

“Swalah! Swalah! Allaah akurehemuni!”

Au wakasema wakati wa kutoa adhaana (الله أكبرَ), (الله آكبر), (الله أكبار) na (الله إكبر). Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Kila Dhikr au du´aa inayofuatia baada ya adhaana ni Bid´ah. Adhaana inatosha kutokana na kila kitu. Jumla inayosema:

الصلاة الصلاة يرحمكم الله

“Swalah! Swalah! Allaah akurehemuni!”

baada ya kumaliza kutoa adhaana ni Bid´ah. Uhakika wa mambo ni kwamba anayesema hivo ni kana kwamba hakuridhika na adhaana iliyosuniwa kuwa kama alama wakati kunapoingia wakati wake.

Kuhusu makosa ya utamkaji, inategemea. Jumla isemayo (الله أكبرَ) haibadilishi maana. Kwa hivyo haiwi ni haramu wala haibatilisha adhaana. Jumla isemayo  (الله آكبر) inabadilisha maana na hivyo haijuzu. Jumla isemayo (الله إكبر) sijui kama inabadilisha maana, lakini kila ambavo inakuwa sahihi zaidi ndio bora.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/197-198)
  • Imechapishwa: 19/03/2026