Swali: Je, Khawaarij ni makafiri?

Jibu: Sio makafiri kwa mujibu wa maoni sahihi. Bali kama alivosema ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh):

“Wamekimbia mbali na ukafiri.”

Maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Wanatoka nje ya dini kama unavyotoka mshale kutoka kwenye upinde wake.”

hakusudii msingi wa dini. Bali anachokusudia (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni sehemu kubwa ya dini yao.

  • Mhusika: Shaykh Swaalih bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://saleh.af.org.sa/sites/default/files/2017-11/0101_0.mp3
  • Imechapishwa: 10/09/2022