Salmaan al-´Awdah na demokrasia

Fitina hizi za mauji ambazo zimesibu miji ya Kiislamu ni natija ya kuwa kwao mbali na Allaah, kutumbukia kwenye fitina na natija ya kutoonelea hadhi ya uhai. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Muumini hatoacha kuwa ni mwenye nafasi ya kufanya matendo mema muda wa kuwa hamwagi damu ya haramu.”

Allaah (´Azza wa Jall) amesema:

مِنْ أَجْلِ ذَٰلِكَ كَتَبْنَا عَلَىٰ بَنِي إِسْرَائِيلَ أَنَّهُ مَن قَتَلَ نَفْسًا بِغَيْرِ نَفْسٍ أَوْ فَسَادٍ فِي الْأَرْضِ فَكَأَنَّمَا قَتَلَ النَّاسَ جَمِيعًا وَمَنْ أَحْيَاهَا فَكَأَنَّمَا أَحْيَا النَّاسَ جَمِيعًا

“Kwa ajili ya hivyo Tukawaandikia wana wa israaiyl kwamba atakayeiua nafsi bila ya nafsi kuua au bila ya kufanya ufisadi katika ardhi, basi ni kama ameua watu wote.” (05:32)

Pamoja na hadhi ya Ka´bah damu ya muislamu ni yenye hadhi kubwa kuliko hadhi ya Ka´bah.

Ni juu yenu kutanabahi:

“Uhai wenu, mali zenu na heshima zenu ni zenye kutakasika kwenu kama mji wenu huu siku yenu hii na mwezi wenu huu.”

Ninakariri na kusema tena kwamba baridi ya kiarabu ambayo inaendelea katika baadhi ya miji ya Kiislamu haikuwaletea Waislamu zaidi ya mabalaa tu. Wale ambao wanaita katika migomo hii wanaita tu katika fitina. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) anasema:

“Mwenye furaha ni yule aliyejikinga na fitina. Mwenye furaha ni yule aliyejikinga na fitina. Mwenye furaha ni yule aliyejikinga na fitina.”

Hapa natumia fursa hii kuwatahadharisha kitabu ambacho ni fitina kwa raia. Mwandishi wacho amekiandika ili kusapoti migomo. Kinaitwa “As-ilat-uth-Thawrah”. Humo huyu mdanganyifu anaita katika migomo. Kinaenezwa katika baadhi ya tovuti na huenda kikapatikana katika baadhi ya maduka ya vitabu. Katika kitabu hichi ameshikilia masuala ya Twaaghuut. Katika hayo anasema:

“Endapo raia watachagua dini nyingine na hukumu isiyokuwa ya Kiislamu basi ni lazima kutumia chaguzi la raia.”

Maneno haya ni kufuru ikiwa anajua hukumu na anajua ni nini hukumu na ni nini maana yake. Kufanya raia ndio wanaohukumu hii ni Twaaghuut. Ni kosa kubwa kusema kwamba ni wajibu kwetu kuhukumiana na sheria ya watu. Sheria ya watu ni Twaaghuut. Maneno kwamba:

“Endapo raia watachagua dini nyingine na hukumu isiyokuwa ya Kiislamu basi ni lazima kutumia chaguzi la raia.”

ni khatari kubwa. Muislamu hasemi hivyo.

Ndugu yetu Shaykh Dr. Fahd bin Sulaymaan al-Fudhayd amemradi kwa Radd inayoitwa “ar-Radd ´alaa As-ilat-ith-Thawrah” na akakataa misingi hiyo haribifu aliyoandika huyu masikini. Ameiradi na kubainisha khatari yake kwa Waislamu. Ni jambo la ajabu vipi mtu atadai kwamba ni katika walinganiaji wanaolingania katika Uislamu kisha anashikilia masuala kama haya khatari ya ki-Twaaghuut. Nimetaja hili ili asije akadanganyika nacho. Huenda mkakipata katika baadhi ya tovuti. Msidanganyike nacho kitabu “As-ilat-ith-Thawrah”. Ni kitabu Twaaghuut. Anaita watu kuhukumu badala ya Shari´ah kuhukumu.

Check Also

Shaykh al-´Adaniy kuhusu ad-Duwaysh, al-Qarniy, al-´Awdah na ash-Shanqiytwiy

Swali: Vipi hali ya watu hawa na je inatakiwa kusikiliza mikanda yao; Ibraahiym ad-Duwaysh, ´Aaidh …