Salamu zote mbili zinafaa

Swali: Ni ipi tofauti kati ya:

السلام عليكم

”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

سلامٌ عليكم

”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”?

Jibu: Yote mawili yanafaa. Bora ni kusema:

السلام عليكم

”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

Ingawa haina neno akisema:

سلامٌ عليكم

”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

 Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipomwandikia Hiraqil alisema:

سلام على من اتبع الهد

”Amani ya Allaah iwe juu ya anayefuata uongofu.”

Makemeo, kama alivyoeleza mshereheshaji aliposema:

سَلَامٌ عَلَىٰ نُوحٍ فِي الْعَالَمِينَ

”Amani iwe juu ya Nuuh ulimwenguni.”[1]

Maneno ya Ibraahiym aliposema:

سَلَامٌ قَوْمٌ مُّنكَرُونَ

”Amani kwa watu wasiotambulikana.”[2]

Kwa hivyo hakuna ubaya.

[1] 37:79

[2] 51:25

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23944/ما-الفرق-بين-السلام-عليكم-وسلام-عليكم
  • Imechapishwa: 02/08/2024