Salamu anapokuwa msalimiwa ni mmoja

Swali: Ni ipi hukumu ya kusema:

السلام عليك

”Amani ya Allaah iwe juu yako.”?

Jibu: Yanafaa yote mawili. Inafaa kusema hivo akiwa ni mtu mmoja. Hata hivyo mara nyingi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisema:

السلام عليكم

”Amani ya Allaah iwe juu yenu.”

Kwa hivyo bora ni hili la pili.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23945/حكم-قول-السلام-عليك-بالافراد
  • Imechapishwa: 02/08/2024