1- Ibn-ul-Madiyniy amesimulia kwamba alimsikia Sufyaan akiulizwa juu ya Ibn Ishaaq na  ni kwa nini watu wa al-Madiynah hawakupokea kutoka kwake. Akasema:

“Nimekaa na Ibn Ishaaq karibu miaka 70. Hakuna yeyote katika watu wa al-Madiynah aliyekuwa anamtuhumu kitu. Hakuna yeyote alikuwa anasema kitu juu yake.” Nikasema: “Ibn Ishaaq alikuwa akiketi na Faatwimah bint al-Mundhir?” Akasema: “Amenipa khabari kwamba amemuhadithia na kwamba aliingia kwake.”

Yahyaa bin Sa´iyd amesema:

“Nimemsikia Hishaam bin ´Urwah akisema: “Ibn Ishaaq amehadithia kutoka kwa mke wangu Faatwimah bint al-Mundhir. Naapa kwa Allaah kwamba kamwe hajawahi kumuona.”

Hishaam ni mkweli katika kiapo chake. Hakumuona, lakini hata mtu huyo hakudai kuwa alimuona. Alichoeleza tu ni kwamba alimuhadithia. Mimi mwenyewe nimesikia kutoka kwa wanawake wengi ingawa sikuwaona. Vivyo hivyo wapo wanafunzi wengi wa Maswahabah waliopokea kutoka kwa ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) na katu hawakuwahi kuona sura yake[1].

2- Ibn Ma´iyn amesema:

“Nimefikiwa na khabari kwamba Shariyk, ath-Thawriy, Israaiyl, Fudhwayl bin ´Iyaadhw na wanachuoni wengine Kuufah walipata watoto Khuraasan. Baba zao walikuwa wakiwatuma huko katika huduma za kijeshi. Baadhi yao wakizaa na wajakazi, wengine wakioa. Wanapomaliza wanaagizwa Kuufah. Masruuq, ndiye babu yake ath-Thawriy, alishuhudia vita vya ngamia.”[2]

[1] 7/38.

[2] 7/242.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 27/01/2021