Swali: Je, imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikusanya Maghrib na ´Ishaa pamoja wakati wa kunyesha mvua?
Jibu: Imethibiti dalili zinazofahamisha hilo. Kwa hiyo hapana vibaya kukusanya swalah ikiwa kuna mvua, khofu au maradhi. Salaf walifanya hivyo ambapo wakakusanya Maghrib na ´Ishaa wakati wa kunyesha mvua. Hili huwa pale ambapo Maghrib inapoadhiniwa hali ya kuwa mvua ni kubwa na yenye kuleta taabu. Ama ikiwa mvua haidhuru au ni ndogo, basi haifai kukusanya swalah. Ikiwa mtu atakusanya katika hali hiyo, basi anatakiwa kuirudia ´Ishaa.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/222)
- Imechapishwa: 16/03/2026
Swali: Je, imethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwamba alikusanya Maghrib na ´Ishaa pamoja wakati wa kunyesha mvua?
Jibu: Imethibiti dalili zinazofahamisha hilo. Kwa hiyo hapana vibaya kukusanya swalah ikiwa kuna mvua, khofu au maradhi. Salaf walifanya hivyo ambapo wakakusanya Maghrib na ´Ishaa wakati wa kunyesha mvua. Hili huwa pale ambapo Maghrib inapoadhiniwa hali ya kuwa mvua ni kubwa na yenye kuleta taabu. Ama ikiwa mvua haidhuru au ni ndogo, basi haifai kukusanya swalah. Ikiwa mtu atakusanya katika hali hiyo, basi anatakiwa kuirudia ´Ishaa.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/222)
Imechapishwa: 16/03/2026
https://firqatunnajia.com/salaf-walikusanya-swalah-wakati-wa-mvua-kali/