Swali:  Je, ipo Hadiyth au masimulizi yanayosema kwamba mtu anayezowea kula nyama ni kama mtu anayezowea kunywa pombe?

Jibu: Kuna masimulizi kutoka kwa baadhi ya Maswahabah kwamba walionya dhidi ya kuendelea kula nyama mara kwa mara na wakasema kwamba ina mtego kama mtego wa pombe. Maana yake ni kwamba mtu akiizoea huwa haiachi kirahisi. Mtu aliyezoea kula nyama hupatwa na pupa juu yake hata kama atajiona ni mtu wa dini. Kwa hiyo inapendeza awe anakula mara na mara nyingine haile, mara anakula nyama na mara haile ili asizoe na isiwe na mtego kwake na asijipee mashaka. Hata hivyo nyama si sawa na pombe. Pombe ni haramu na nyama ni halali. Lakini kusudio ni kwamba mtu anapozowea sana, baadhi ya Salaf walikuwa wakichukia kuizoea kupita kiasi na wakisema inapasa awe anakula mara kwa mara tu, si kila siku, ili asizowee na asijiletee uzito juu ya nafsi yake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/2399/هل-ورد-اثر-ان-المدمن-في-اكل-اللحم-كمدمن-الخمر
  • Imechapishwa: 28/03/2026