Salaf hawakuwa wakiandika Aayah za Qur-aan misikitini na majumbani

Swali: Ni ipi hukumu ya kuandika Aayah za Qur-aan na kuzibandika katika misikiti au majumbani?

Jibu: Haifai. Dogo kabisa liwezalo kusemwa ni kwamba inachukiza, kwa sababu huwafanya wanaoswali washughulike, kuwakera na huwavuruga. Misikiti inapaswa iwe salama kutokana na mambo haya ili wanaoswali wasishughulishwe na visomo, maandishi na michoro iliyo kwenye kuta.

Swali: Hata katika majumbani pia?

Jibu: Hapana. Majumbani ni mepesi zaidi, lakini misikiti ndiyo inapaswa itakaswe na mambo haya ili yasiwashughulishe wanaoswali. Ama majumbani jambo lake ni pana zaidi.

Swali: Huenda Aayah zikamkumbusha swalah au unyenyekevu?

Jibu: Salaf wetu hawakuwa wakifanya jambo hili katika misikiti.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1936/حكم-تعليق-الايات-القرانية-على-جدران-المساجد-والبيوت
  • Imechapishwa: 28/12/2025