Swali: Ni ipi hukumu ya maigizo ya Kiislamu?
Jibu: Ni haramu. Dogo liwezalo kusemwa ni kwamba ni uwongo. Mwigizaji anadai kuwa yeye ni Abu Jahl, Khaalid bin al-Waliyd au ´Aliy bin Abiy Twaalib. Baya zaidi kuliko hayo ni kwamba pengine akamwigiza shaytwaan ambaye anawashawishi watu. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kujifananisha na shaytwaan. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Anapokula mmoja wenu, basi ale kwa mkono wake wa kuume. Na anapokunywa mmoja wenu, basi anywe kwa mkono wake wa kuume; kwani hakika shaytwaan anakula na kunywa kwa mkono wake wa kushoto.”
Maigizo yana maana ya kujifananisha na makafiri. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kujifananisha na makafiri:
“Yeyote mwenye kujifananisha na watu, basi yeye ni katika wao.”[1]
Ni uwongo kusema kuwa maigizo ni katika njia za ulinganizi. Hayakuthibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Maswahabah, wanafunzi wa Maswahabah. Uhakika wa mambo ni kwamba maigizo, maandamano na mambo mengine ya sasa ni yenye kutoka kwa maadui wa Uislamu. Kunakhofiwa waigizaji wakaingia ndani ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Watu aina tatu ndio wenye adhabu kali siku ya Qiyaamah: kiongozi mpotofu, mtu aliyemuua Nabii au akauliwa na Nabii na mwigizaji.”[2]
Anakusudiwa mwigizaji anayemwigliza mwingine au ni mtengenezaji picha? Yote mawili yanawezekana. Kwa mujibu wa kiarabu neno hilo linakusanya wote wawili.
Walipokosa elimu ya Qur-aan na Sunnah, ndipo wakayaelekea maigizo haya.
[1] Ahmad (5114, 5115 na 5667), al-Khatwiyb katika ”al-Faqiyh wal-Mutafaqqih” (2/73) na Ibn ´Asaakir (1/96).
[2] Ahmad.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 393-394
- Imechapishwa: 23/06/2025

Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 393-394
Imechapishwa: 23/06/2025
https://firqatunnajia.com/salaf-hawakufanya-maigizo/