Imaam an-Nawawiy (Rahimahu Allaah) amesema:

160 – an-Nu´maan bin Bashiyr (Radhiya Allaahu ´anhumaa) ameeleza ya kwamba nilimsikia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)  akisema:

واللهِ لَتُقِيمُنَّ صفوفَكم أو ليُخالِفَنَّ اللهُ بينَ قلوبِكم

“Ninaapa kuwa mtazipanga safu zenu au Allaah atatia uadui kwenye mioyo yenu.”[1]

Lau mtu atauliza ikiwa kama kuna imamu na maamuma tu, imamu ajongee kwa mbele kidogo au wasimame sawa sawa katika safu moja? Wapange safu sawa. Kwa sababu ikiwa ni yeye na maamuma safu inakuwa ni moja. Maamuma hawezi kusimama peke yake nyuma ya imamu. Bali watafanya safu moja. Safu moja wanatakiwa kusimama sawa sawa. Ni tofauti na walivosema baadhi ya wanachuoni ya kwamba imamu anatakiwa kusogelea mbele kidogo. Hili halina dalili. Dalili zinaonesha kinyume na hivo. Dalili zinaonesha kuwa imamu na maamuma wanatakiwa kupanga safu sawa ikiwa ni wao wawili tu.

[1] al-Bukhaariy na Muslim

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/289-290)
  • Imechapishwa: 18/12/2024