Sababu ya mwanzoni mwa Uislamu kukatazwa kuyatembelea makaburi

Swali: Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Nilikuwa nimewakataza kuyatembelea makaburi… ”

Jibu: Mwanzoni walikuwa wamekatazwa kuyatembelea makaburi, kisha katazo hilo likafutwa. Hii ni kwa sababu walikuwa wapya katika Uislamu, hivyo wakakatazwa kuyatembelea makaburi ili kuepusha kutokea kwa shirki yoyote. Lakini baada ya Uislamu kuthibitika katika nyoyo zao na wakauelewa, basi wakaruhusiwa kuyatembelea makaburi. Kwa sababu sasa kuna manufaa bila madhara. Kutembelea makaburi kunalainisha nyoyo na kukumbusha kifo na Aakhirah.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/28809/هل-كانت-زيارة-القبور-ممنوعة-ثم-رخص-فيها
  • Imechapishwa: 25/04/2025