Swali: Vipi kufasiri swalah kwamba ni rehema?

Jibu: Hapana. Kuswalia kwa Allaah ni kusifu. Husemwa kwamba Allaah anawaswalia waja Wake (صلاة على عباده). Lakini ndani ya swalah kunaingia pia rehema. Amesema (Ta´ala):

أُولَـٰئِكَ عَلَيْهِمْ صَلَوَاتٌ مِّن رَّبِّهِمْ وَرَحْمَةٌ

“Hao zitakuwa juu yao sifa kutoka kwa Mola wao na rehema.”[1]

Rehema hapa ni kuwafanyia ihsani na swalah ni kuwasifu. Swalah inapotajwa kwa kuachia kunaingia pia rehema:

هُوَ الَّذِي يُصَلِّي عَلَيْكُمْ وَمَلَائِكَتُهُ

“Yeye ndiye anakusifuni na Malaika Wake wanamuomba akughufurieni.”[2]

Kwa maana ya kwamba anawasifu na kuwarehemu kwa rehema Zake. Hapa ni pale ambapo inatajwa kwa kuachia.

[1] 02:157

[2] 33:43

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydah al-Waasitwiyyah (01)
  • Imechapishwa: 12/05/2024