Swali: Anauliza kuhusu mavazi yenye kubana, sidiria za matiti na rangi nyekundu ya mdomo?
Jibu: Mavazi ya kubana hayajuzu kwa mwanamke kuyavaa isipokuwa kama atakuwa nyumbani kwake na asiwepo zaidi ya mume wake. Hilo ni kwa sababu mavazi ya kubana yanayoonyesha fumo ya mwili ukweli wa mambo ni kwamba yanazingatiwa kuwa ni yenye kusitiri ilihali si yenye kusitiri. Ni yenye kusitiri kwa njia ya kwamba yameficha rangi ya mwili. Lakini si yenye kusitiri kwa njia ya kwamba fomu ya mwili yaonekana. Kitendo hicho kinaingia ndani ya maneno ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona; wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, Maaylaat na Mumiylaat. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”
Kisha baada ya hapo akataja wanawake waliovaa na wakati huohuo wako uchi. Mwanamke huyu ambaye amevaa mavazi yenye kubana yanayoonyesha fomu ya mwili ukweli wa mambo ni kwamba amevaa lakini yuko uchi. Hivyo haijuzu kwake kuvaa mavazi kama haya muda wa kuwa hayuko nyumbani ambapo hakuna zaidi ya mume wake.
Kuhusu sidiria hazina neno. Isipokuwa mimi naona kuwa haitakiwi kwa mwanamke kijana ambaye hajaolewa kuivaa. Kwa sababu hapo ndipo ataanza kukuwa hali ya kupenda kuonekana na kujiweka katika mitihani. Hivyo haitakiwi kwake kuivaa. Hakuna neno kwa mwanamke ambaye ni mke wa mtu ambaye anamvalia mume wake. Ni katika kujipamba.
Ama rangi nyekundu ya mdomoni ni katika mambo ambayo kwayo mwanamke hujipamba. Ni kama hina kwenye mikono na kwenginepo. Msingi ni kujuzu. Kama kumepokelewa kitu kinachopelekea katika uharamu Allaah ndiye anajua zaidi.
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Nuur ´alaad-Darb (16) http://binothaimeen.net/content/6812
- Imechapishwa: 23/03/2021
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Mavazi yenye kubana kati ya wanawake wenziwe
Swali: Wanawake wengi wanavaa mavazi ya sketi na blauza na yanakuwa yenye kubana kidogo lakini si yenye kuonyesha kwa ndani na si mafupi. Ni ipi hukumu ya mavazi haya? Jibu: Mwanamke wa kiislamu anatakiwa kumcha Allaah juu ya mavazi yake na mavazi yake yawe yenye kusitiri na yasiwe yenye kuonyesha ndani bi…
In "Jumla kuhusiana na vazi la mwanamke"
Mavazi yanayoonyesha ndani
Swali: Vipi kuhusu mavazi ya kuonyesha ndani? Jibu: Hapana, mavazi ya kuonyesha ndani hayajuzu. Mavazi ya kuonyesha ndani ni ya khatari yanaweza kuonyesha uchi. Lakini ikiwa ni mavazi ya kuonyesha ndani mikono jambo ni jepesi kidogo muda wa kuwa sehemu nyingine ya mwili imefunikwa vizuri. Ni lazima mavazi yawe yenye kusitiri na…
In "Jumla kuhusiana na vazi la mwanamke"
24. Sifa za vazi la Kishari´ah la mwanamke wa Kiislamu
1 - Ni lazima kwa vazi la mwanamke wa Kiislamu liwe pana linalomfunika mwili wake mzima mbele ya wanaume ambao sio Mahram zake. Asijifunue mbele ya Mahram zake mbali na yale ambayo kidesturi yamezoeleka kufunuliwa kama vile uso wake, viganja vyake vya mikono na miguu yake. 2 - Liwe ni…
In "04. Sura ya nne: Hukumu zinazohusu mapambo na Hijaab"