Rak´ah nne au mbili kabla ya Dhuhr?

Swali: Je, bora mtu aswali Rak´ah nne kabla ya Dhuhr au Rak´ah mbili?

Jibu: Rak´ah nne kabla ya Dhuhr ambazo ni Raatibah. Hivi ndio bora na ndio kamilifu zaidi. ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) amesema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa haachi Rak´ah nne kabla ya Dhuhr.”

Swali: Vipi ikiwa wakati fulani anaswali Rak´ah mbili?

Jibu: Hapana vibaya. Hata hivyo Rak´ah nne ndio bora zaidi. Dumu kuswali Rak´ah nne.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/22542/ما-الافضل-في-عدد-ركعات-الراتبة-قبل-الظهر
  • Imechapishwa: 04/07/2023