Rak´ah mbili za Sunnah au swalah ya Fajr?

Swali: Nikiamka katika swalah ya Fajr nimechelewa nitangulize Rak´ah mbili zinazokuwa kabla ya swalah hata kama ninakhofia kuchomoza kwa jua?

Jibu: Ndio, hili ni lazima. Tanguliza Rak´ah mbili za kabla ya swalah. Hivi ndivyor alivofanya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Lakini ni kitu gani kilichokufanya kuchelewesha Fajr? Jimaa ndio inakufanya kuchelewesha Swalah? Ikiwa umezidiwa na wewe hukukusudia, unapewa udhuru. Ama ikiwa huu ndio mtindo wako, hili ni kosa kubwa. Kwanza unaacha swalah ya mkusanyiko. Pili unaitoa swalah nje ya wakati wake kwa sababu ya upuuzaji wako.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Qaa´idah Jaliylah fiyt-Tawassul wal-Wasiylah (05) http://www.alfawzan.af.org.sa/node/2124
  • Imechapishwa: 01/07/2020