Qur-aan haikuletwa ili itundikwe kwenye ukuta

Swali: Ni ipi hukumu ya kutundika baadhi ya Aayah za Qur-aan au Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwenye mabango ndani ya nyumba ni ipi?

Jibu: Fatwa tunayotoa ni kwamba hili halijuzu, kwa sababu hili linapelekea kuanguka na kuonekana kama kutoheshimu maandiko hayo. Aidha kwa sababu Qur-aan haikuteremshwa ili itundikwe ukutani, katika kuta za misikiti au nyumba. Bali imeteremshwa ili ifanyiwe kazi na ihifadhiwe. Hii ndiyo hekima ya kuteremshwa kwake, si kutundikwa kwenye kuta, misikitini au yenye kufanana na hivyo. Basi lililopasa ni kutokufanya hivyo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1090/حكم-تعليق-لوحات-فيها-ايات-قرانية-داخل-البيوت
  • Imechapishwa: 24/01/2026