Jipime maarifa yako kuhusu wudhuu´ na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah
15:00
Je, mtu aliye na hadathi ndogo anaruhusiwa kuswali kabla ya kutawadha?
- Ndio, anaruhusiwa ikiwa hana maji
- Hapana, haruhusiwi kuswali bila wudhuu'
- Anaweza kuswali ikiwa atataja jina la Allaah
Je, inasihi swalah ya Maghrib kwa imamu aliyesoma kimyakimya?
- Ndio, inasihi
- Hapana, haisihi lazima asome kwa sauti ya juu
- Lazima kwa imamu arudi kuswali na si maamuma
Je, ni lazima kwa wanaume kuswali msikitini?
- Ndio, ni lazima kuswali kwa mkusanyiko kila swalah
- Hapana, si lazima bali inapendeza tu
- Inaruhusiwa kuswali nyumbani kwa hali yoyote
Je, inafaa kuanza kuswali swalah ya Sunnah baada ya kukimiwa swalah msikitini?
- Ndio, anaweza kuswali kwanza sunnah
- Hapana, anapaswa kuungana na imamu kwanza
- Anaweza kuswali sunnah pembeni mwishoni
Je, inafaa kuswali na viatu?
- Hapana, hayo ni matendo ya manaswara makanisani
- Ndio, bali kufanya hivo ni Sunnah
- Ndio, kwa sharti viatu viwe viapya
Je, mtu anayeswali kwa kufuata imamu swalah ya kimyakimya lazima asome al-Faatihah katika kila Rakaa?
- Ndio, lazima asome
- Hapana, si lazima
- Anaweza kusoma Aayah yoyote badala ya al-Faatihah
Je, inafaa kuvunja swalah ikiwa mtu ametilia shaka kuchengukwa kwa wudhuu?
- Hapana, mpaka uwe na uhakika wa kuchengukwa na wudhuu´ wako
- Ndio, lazima uvunje swalah yako
- Swalah yako haisihi mpaka utawadhe tena
Je, ni ruhusa kuswali bila wudhuu ikiwa hakuna maji wala udongo wa Tayammum?
- Ndio, ni ruhusa kuswali
- Hapana, si ruhusa kuswali
- Unaweza kuswali kwa nia bila Tayammum
Je, swalah ya mtu ambaye anaweza kuswali kwa kusimama lakini anapendelea kuswali kwa kukaa inakubaliwa?
- Ndio, itakubalika kwa sababu ya nia nzuri
- Hapana, haitakubalika ikiwa anaweza kusimama
- Itakubalika ikiwa ataswali kwa muda mrefu
Je, mtu aliye na udhuru wa kiafya anaweza kuswali kwa kukaa hata kama anaweza kusimama kwa shida?
- Ndio, anaweza kuswali kwa kukaa ikiwa atasikia maumivu makali
- Hapana, lazima asimame hata kama ni kwa shida
- Ni bora aswali kwa ishara za mwili bila kutumia viungo
Vipi swalah ya mswaliji anayetokwa na damu?
- Ndio, swalah imebatilika mara moja
- Hapana, haibatiliki ikiwa damu ni kidogo
- Damu yenye kutoka puani pekee ndio inaharibu swalah
Nini anachotakiwa kufanya mswaliji ambaye ameingiwa na shaka kama ana wudhuu au laa?
- Ajengee yuu ya yakini na aendelee kuswali
- Arudi akachukue wudhuu' upya
- Aombe du'aa ya msamaha na kuendelea
Ni ipi hukumu ya swalah ya ambaye amesahau akaswali na nguo yenye najisi?
- Swalah yake ni sahihi na hatoirudi
- Hana swalah na lazima airudi
- Swalah yake inasihi tu kama ni ya Sunnah na si faradhi
Je, mtu anaweza kuswali swalah ya Dhuhr kabla ya muda wake kwa sababu ya safari?
- Ndio, anaweza kuswali kabla ya muda kwa safari
- Hapana, hawezi kuswali kabla ya muda wake
- Anaweza kuswali ikiwa anahisi atachelewa sana
Ni ipi hukumu ya ambaye baada ya swalah amekumbuka hakutawadha?
- Swalah yake ni sahihi na hatoirudi
- Swalah yake si sahihi na lazima atawadhe na airudi
- Swawm yake ni sahihi kwa.s amesahau
Je, inajuzu kwa mgonjwa asiyeweza kuswali kila swalah kwa wakati kukusanya swalah?
- Haijuzu, lazima kila swalah ndani ya wakati wake
- Inajuzu kukusanya Dhuhr na ´Aswr, Maghrib na ´Ishaa
- Inajuzu kukusanya swalah zote wakati mmoja
Je, swalah ya mkusanyiko inakuwa batili ikiwa imamu anafanya makosa katika al-Faatihah?
- Ndio, swalah inakuwa batili ikiwa ni kosa la kubadilisha maana
- Hapana, swalah haibatiliki kwa kosa dogo lisilobadilisha maana
- Lazima swalah irudiwe na waumini wote
Je, inakubaliwa swalah ya ambaye amesahau kusoma al-Faatihah?
- Ndio, inakubalika kwa sababu ni amesahau
- Hapana, haikubaliki bila al-Faatihah
- Anaweza kuswali suujud ya kusahau pekee
Je, inafaa kwa mtu kuswali bila kuvaa nguo ya chini (ya ndani) ikiwa nguo yake ya juu inafunika mwili wake wote?
- Ndio, inafaa kuswali ikiwa amejifunika vyema
- Hapana, haifai na swalah haisihi
- Anaweza kuswali kwa kuweka leso miguuni
Je, ni sahihi kumfuata imamu katika swalah ikiwa unajua ana hadathi?
- Ndio, ni sahihi kumfuata
- Hapana, si sahihi kumfuata ikiwa ana hadathi
- Unaweza kumfuata ikiwa amevaa nguo safi
Je, ni ruhusa kuchelewesha swalah ya Maghrib hadi muda wa Ishaa ikiwa hauna udhuru?
- Ndio, ni ruhusa kuchelewesha hadi muda wa 'Ishaa
- Hapana, si ruhusa kuchelewesha bila udhuru
- Inaruhusiwa ikiwa unajishughulisha na kazi
Je, inasihi swalah ya ambaye amepinda kidogo na Qiblah?
- Hapana, haisihi kabisa
- Ndio, inasihi kama ni kidogo tu
- Lazima aanze swalah upya