Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah 08
15:00
Inafaa kupangusa juu soksi na khofu nyembamba?
- Hapana na twahara haisihi
- Inafaa tu kama zinafunika macho ya miguu
- Ndio, inafaa muhimu hazionyeshi ndani ya mguu kana kwamba uko wazi
Ni lini unaanza kuhesabiwa muda wa kupangusa juu ya soksi na khofu?
- Pale anapofikiria kuzivaa
- Pale anapopangusa mara ya kwanza au pale anapopata hadathi ya kwanza baada ya kuzivaa
- Pale anapoanza kuswali swalah ya kwanza baada ya kuzivaa
Kipi ni sahihi katika haya?
- Ili ifae kupangusa juu ya soksi ni lazima mtu awe alizivaa wakati yuko na twahara
- Baada ya kuswali swalah tano haifai kuendelea kupangusa juu ya soksi
- Soksi zinapanguswa kwa chini tu na si kwa juu
Nini afanye mtu ambaye anataka kufanya tendo la ndoa na hakuna maji?
- Lazima asubiri mpaka kupatikane maji
- Akifanya na anajua hakuna maji anapata dhambi
- Afanye kisha atafanya Tayammum
Ni kipi katika mambo haya ni nguzo ya swalah?
- Kusema (Rabbana walakal hamd)
- Kuinuka kutoka kwenye Rukuu'
- Kusoma kwa sauti ya juu katika Fajr
Swalah inampasa kafiri ambaye amesilimu punde kdg na hajui Suurah hata moja?
- Hapana, huyo ana udhuru
- Ataanza kuswali akishajua al-Faatihah
- Anapaswa kusoma na ataleta Adhkaar katika swalah yake
Ni ipi hukumu ya kukusanya dua ya kufungulia swalah zaidi ya moja katika swalah moja?
- Inapendeza kufanya hivo
- Haifai kufanya hivo
- Mtu anapata malipo zaidi
Vipi twahara ya ambaye amepangusa baada ya kumalizika muda uliopangwa na Shariah?
- Twahara inasihi kama amesahau
- Twahara haisihi hata kama amesahau
- Itategemea twahara hiyo anaifanyisha 'ibaadah gani
Nini anachofanya mgonjwa asiyeweza kutawadha?
- Ataswali bila kutawadha
- Atatawadhishwa na mtu
- Ataanza kuswali wakati ataweza kutawadha
Ni ipi hukumu ya kuswali nyuma ya wazushi?
- Haifai
- Swalah haisihi kabisa
- Sahihi ni kwamba swalah inasihi muda wa kuwa ni waislamu
Ni lini wanapigwa watoto wanapokataa kuswali?
- Miaka saba
- Miaka tano
- Miaka kumi
Ni kweli kwamba muda wa swalah ya usiku unaanza baada ya Maghrib?
- Hapana, ila kwa msafiri tu
- Ndio, katika baadhi ya hali
- Unaanza baada ya 'Ishaa katika hali zote
Inafaa kupangusa juu soksi na khofu zisizofunika kongo mbili za miguu?
- Ndio, kama ni kubwa na pana
- Ndio, kama ndio soksi pekee alizonazo
- Hapana haifai
Ni muda kiasi gani msafiri anatakiwa kupangusa juu ya soksi na khofu?
- Masaa kumi na mbili
- Masaa sabini na mbili
- Masaa ishirini
Nini kinachompasa ambaye yuko na maji lakini hawezi kuyatumia?
- Atasubiri mpaka atapoweza
- Hana wajibu wa kuswali kwa.s ana udhuru
- Atafanya Tayammum
Ni muda kiasi gani ambaye si msafiri (mkazi) anatakiwa kupangusa juu ya soksi na khofu?
- Masaa sabini na mbili
- Masaa ishirini na nne
- Masaa kumi na mbili
Ni kipi katika mambo haya ni katika sharti za swalah?
- Nia
- Kutoa salamu kuliani na kushotoni
- Kutia mikono miwili juu ya kifua
Ni kwanini imesuniwa kusoma Suurah ndefundefu Fajr?
- Kuwaondoa watu usingizi
- Ndio Sunnah, na pia ni kisomo kinachoshuhudiwa na Malaika
- Kwa ajili ya kuiga swalah za Mitume
Nini anachotakiwa kufanya mtu anapokumbuka ndani ya swalah kuwa nguo zake zina najisi?
- Atavunja swalah na hakuna namna nyingine
- Ataivua nguo hiyo kama inawezekana kisha endelee na swalah yake
- Ataanza upya swalah yake
Ni viungo vipi katika wudhuu ni lazima vioshwe?
- Kuosha uso, mikono mpaka kwenye visugudi, kupangusa kichwa na miguu hadi vifundoni
- Kuosha uso na miguu
- Kuosha viganja vya mikono na kupangusa kichwa
Ni kipi katika mambo haya ni katika sharti za swalah?
- Kusoma al-Faatihah
- Mtu kuondosha najisi
- Kuswali kwa unyenyekevu