Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah

Chemsha Bongo ya twahara na swalah 05

15:00

Ni wapi pa kuangalia wakati umekaa kwenye Tashahhud?

  • Mbele yako
  • unamtazama imamu

Mwanzoni wakati Mtume alipopewa swalah zilikuwa ngapi kwa siku?

  • 15
  • 100

Inafaa kuirudia swalah ya Istikhaarah?

  • Ndio, kama mtu hujabainikiwa
  • Inafaa tu kama aliiswali kimakosa

Je, kipi katika haya ni mojawapo ya nguzo za swalah?

  • Kusoma kwa sauti ya juu
  • Sujuud

Ni swalah ipi katika hizi inaitwa Awwaabiyn?

  • Dhuhaa
  • Istisqaa'
  • Witr

Ni viungo vingapi ambavyo mtu anaposujudu vyote vinatakiwa kugusa ardhi?

  • 5
  • 7

Ni ipi hukumu ya kuweka kitu juu ya paji la uso wakati wa kusujudu?

  • Ni Sunnah
  • Inachukiza kufanya hivo kama hakuna dharurah

Ni ipi hukumu ya kuswali kwa kuelekea moto?

  • Inapendeza
  • Ni jambo limehimizwa

Ni ipi hukumu ya kuswali kwa kufumba macho kwa madai ya unyenyekevu?

  • Inachukiza
  • Inapendeza

Je, inasihi mtu mkubwa kuswalishwa na mtoto?

  • Inafaa tu kama amehifadhi Qur-aan yote
  • Ndio, inafaa kama ameshabaleghe

Ni Mtume gani alimshauri Mtume wetu Muhammad arudi kwa Allaah kumuomba ampunguzie idadi ya swalah alizokuwa amepewa mwanzoni?

  • Muusa
  • Aadam

Ni wapi pa kuangalia wakati mtu amesimama na kuswali?

  • Mahali unaposujudia
  • Mbele yako

Ni ibaadah ipi pekee ambayo Mtume alipanda juu mbinguni kuipokea moja kwa moja kutoka kwa Allaah?

  • Swalah
  • Swawm

Ni swalah ipi katika hizi ina Rukuu mbili kwenye Rakah zake zote mbili?

  • Istikhaarah
  • Kusuuf

Ni ipi hukumu ya ambaye katika swalah za kusoma kimyakimya amesoma kwa sauti ya juu?

  • Swalah yake inabatilika
  • Swalah yake ni sahihi lakini amekhalifu Sunnah

Ni ipi hukumu ya kupangusa uso baada ya kumaliza kuomba dua?

  • Lazima kufanya hivo
  • Hadiyth zake haijathibiti

Ni ipi hukumu ya anayekusudia kuosha viungo vya wudhuu vyote au baadhi mara moja badala ya mara tatu?

  • Wudhuu' wake una mapungufu
  • Wudhuu' wake ni sahihi

Ni ipi hukumu ya kuomba dua kwa kunyanyua mikono juu baada ya swalah tano za faradhi?

  • Bid'ah
  • Du'aa inaitikiwa haraka

Je, inafaa kukusanya swalah ya Sunnah Rakah nne kwa salamu moja?

  • Inafaa ijapo bora ni kutofanya hivo
  • Inafaa tu kama ni swalah ya Sunnah

Ni ipi hukumu ya kuswali kwa kuelekea picha?

  • Haina neno kabisa
  • Inachukiza

Ni ipi hukumu ya kuleta dua za pamoja baada ya swalah?

  • Bid'ah
  • Sunnah ya Mtume

Vipi twahara ya ambaye hadathi yake ni yenye kudumu?

  • Ataoga wakati wa kila swalah
  • Ataoga na kutawadha