Jipime maarifa yako kuhusu swawm
Chemsha Bongo ya Ramadhaan 10
15:00
Mtu afunge na mwezi wa kuonekana popote au afunge na mwezi wa mji wake tu?
- Hakuna mwezi wa popote ni Bid'ah
- Mtu afunge na mwezi wa mji wake tu na hakuna mwezi wa popote
- Wanazuoni wametofautiana tangu hapo kale na mtu afuate yale maoni anayoona kuwa na nguvu zaidi
Ni Suurah ipi ndani ya Qur-aan iliyotaja kwamba swawm ilikuwa imefaradhishwa kwa watu waliokuwa kabla yetu?
- al-Ahzaab
- at-Tawbah
- al-Baqarah
Je, inafaa mwanamke kutumia dawa ya kuzuia hedhi ili aweze kufunga Ramadhaan?
- Ndio inafaa, japo bora ni kuepuka hilo kwa sababu za kiafya
- Haifai ni haramu
- Ndio, inafaa tu kama ni vidonge alivyoandikiwa na daktari na si mitishamba
Imesuniwa kuipokea Ramadhaan vipi?
- Kwa dufu na kuimba Anaashiyd
- Kwa kusoma maulidi
- Kwa furaha, kutubia na kujiandaa kufanya 'ibaadah mbalimbali
Ni ipi hukumu ya kuunganisha swawm (kufunga bila kula daku) siku 2 au zaidi?
- Ni haramu na swawm haisihi
- Inafaa Mtume kafanya hivo, lakini inachukiza
- Mtu anapata thawabu mara mbili
Swawm ipi iliyokuwa wajibu kufunga hapo kabla ya kufaradhishwa funga ya Ramadhaan?
- Swawm ya 'Arafah
- Swawm ya j.tatu na alkhamisi
- Swawm ya 'Aashuuraa'
Ni Suurah ipi ndani ya Qur-aan iliyotaja kwamba kufunga Ramadhaan ni wajibu?
- al-Maaidah
- al-Baqarah
- Aal ´Imraan
Ni ipi hukumu ya wale wanaomsha watu kula daku kwa kupiga ngoma na makelele?
- Ni Bid'ah
- Haina neno ni kusaidiana katika wema
- Wanaofanya hivo wanapata malipo makubwa
Vipi swawm ya ambaye amevuta kamasi za mtoto mchanga mwenye matatizo ya kupumua (nimonia)?
- Ni sahihi muhimu asimeze
- Si sahihi na apaswa kufunga siku nyingine
- Atafunga siku nyingine na kutoa kafara kwa kuharibu funga yake
Je, mwanamke kujipodoa kunaharibu swawm?
- Ndio, kwa.s vina kemikali
- Hapana, kwa.s si kula wala kunywa
- Ndio, kama atajipura sana usoni na akahisi harufu yake kooni
Vipi swawm ya mwanamke ambaye ameenda kufanyiwa matibabu kwenye uke wake na daktari wa kiume?
- Hana swawm na lazima alipe siku nyingine
- Swawm yake ni sahihi
- Swawm yake ina mapungufu ijapo ni sahihi
Ni mlango upi wa Pepo unaofunguliwa unapoanza mwezi wa Ramadhaan?
- Mlango wa ar-Rayyaah
- Ni milango yote 8 ya Pepo
- Ni mlango wa wafungaji
Je, ni lazima kukaa Itikaaf kumi lote la mwisho au mtu anaweza kukaa Itikaaf baadhi ya nyakati za mchana au usiku?
- Ndio, lazima mtu hawezi kukaa I'tikaaf
- Hapana, mtu anaweza kukaa baadhi ya nyakati
- I'tikaaf lazima kumi lote, la sivyo mtu asikae
Vipi kwa aliyekaa Itikaaf kuzungumza na simu?
- Haipendezi ila kama kuna dharurah
- Haifai kabisa akiongea I'tikaaf imeharibika
- Hakuna tatizo lolote kuongea na simu wakati wa I'tikaaf
Kipi kilichosihi katika haya?
- Harufu ya mfungaji ni nzuri kushinda harufu ya udi
- Harufu ya mfungaji ni nzuri kushinda harufu ya marashi
- Harufu ya mfungaji ni nzuri kushinda harufu ya miski
Ni vipi ilikuwa swawm ya Nabii Daawuud ambayo Mtume amesema ndio funga bora?
- Ni kufunga jumatatu na alkhamisi
- Kufunga masiku meupe
- Kufunga siku moja na kula siku inayofuata
Ni msikiti wenye sifa zipi ambao mtu anatakiwa kukaa Itikaaf?
- Msikiti wa Shaykh mkuu wa mji
- Msikiti wenye darsa mara kwa mara
- Msikiti ambao unaswaliwa faradhi tano, ijumaa, una choo n.k. kwa namna ya kwamba mtu hatohitaji kutoka bila dharurah
Nini makusudio ya kwamba Mtume katika 10 la mwisho alikuwa akihuisha nyusiku zake?
- Alikuwa anakesha akijipinda kuutafuta usiku wa Qadr
- Alikuwa akilala sehemu kubwa ya usiku na akisimama sehemu nyingine iliyobakia
- Alikuwa akilala nusu ya usiku na akiswali nusu nyingine
Je, anapaswa kutoa kafara mwanaume ambaye amemwaga manii baada ya kufanya romantik na mkewe?
- Ndio, kwa.s ameharibu swawm yake
- Hapana hatotoa kafara na hahitajiki kufunga siku nyingine
- Hapana hatotoa kafara, ila swawm yake imeharibika na hivyo lazima afunge siku nyingine
Ni Suurah ipi ndani ya Qur-aan iliyoruhusu wanandoa kujamiiana usiku wa Ramadhaan?
- al-Baqarah
- al-Nisaa'
- an-Nuur
Ni usiku gani katika Ramadhaan ambao watu huachwa huru na Moto?
- Ni kila usiku wa Ramadhaan
- Ni usiku wa tarehe 27 Ramadhaan
- Ni usiku wa kila ijumaa Ramadhaan
Ni mlango upi wa Moto unaofungwa unapoanza mwezi wa Ramadhaan?
- Mlango wa wasiofunga
- Ni mlango wa wazinzi Ramadhaan
- Milango yote ya Moto hufungwa