Jipime maarifa yako kuhusu swawm
Chemsha Bongo ya Ramadhaan 08
15:00
Inafaa kuswali swalah ya usiku kwa kuketi chini swalah ikimlemea?
- Hapana
- Ndio, ila ajitahidi kusimama wakati wa al-Faatihah
- Inafaa kwa wazee na wagonjwa tu na si vijana
Inafaa kwa msafiri wa ndege kula ikiwa hapati uzito wowote kufunga?
- Haifai kwa hali yoyote
- Inafaa midhali ni msafiri
- Inafaa tu wakati atapokuwa njiani na si baada ya kufika anakoenda
Ni wajibu kwa imamu kukhitimisha Qur-aan katika Tarawiyh?
- Ndio, ni wajibu
- Hapana, si wajibu
- Ni wajibu katika Tahajjud na si Tarawiyh
Je, ipi hukumu ya mwanamke mwenye hedhi kusoma tafsiri ya Qur-aan?
- Ni haramu
- Inafaa
- Lazima ashike nyuma ya jalada
Kipi kilichosihi katika haya?
- Asiyewaheshimu wazazi hana Pepo
- Pepo iko chini ya miguu ya wazazi
- Ameangamia ambaye amediriki Ramadhaan na asisamehewe madhambi yake
Ni yepi katika haya kilichosihi?
- Malipo ya siku moja ya swawm ni sawa na thawabu 70
- Malipo ya swawm ni sawa na mlima wa Uhud
- Swawm ni ya Allaah, Naye ndiye atakayeilipa
Je, inafaa kwa mume kumjamii mkewe katika swawm yake ya kulipa Ramadhaan?
- Inafaa kwa.s haki ya mume ni kubwa ziaidi
- Haifai na mume atatoa kafara
- Haifai na mume ana dhambi kumuharibia swawm yake
Je, mwanafunzi anayo ruhusa ya kuacha kufunga kwa sababu ya mitihani ya shuleni?
- Hana ruhusa
- Anayo ruhusa tu kama ni masomo ya kiislamu
- Anayo ruhusa lakini anatakiwa kulipa siku nyingine
Mfungaji anakuwa na furaha mbili wakati gani?
- Wakati wa kusoma Qur-aan na kutoa swadaqah
- Wakati wa kufungua na wakati atapokutana na Mola wake
- Wakati wa kuingia Peponi na wakati wa kupewa daftari lake siku ya Qiyaamah
Kipi kilichosihi katika haya?
- Du'aa ya mfungaji inaitikiwa wakati wote
- Wakati wa futari peke yake
- Wakati wa daku
Vipi swawm kwa mtoto ambaye amebaleghe mchana wa Ramadhaan?
- Ataendelea kula na kunywa na kuanza kufunga siku inayofuata
- Atajizuia siku hiyo na kuanza kufunga siku inayofuata
- Ataanza kufunga Ramadhaan ya mwaka unaofuata
Ni ipi hukumu ya kujizuia kula dakika 15 (imsaak) kabla ya adhaana ya Fajr?
- Lazima kujizuia
- Si lazima bali ni Bid'ah
- Akila mpaka wakati wa adhaana anapaswa kutoa kafara
Nini kinachompasa mzee anayeweza kufunga baadhi tu ya siku za Ramadhaan?
- Ataacha kufunga na kulisha masikini 30
- Ataacha huru watumwa 30
- Atafunga zile siku anazoweza na atalisha masikini kwa idadi ya siku zilizomshinda
Qur-aan imeanza kushushwa…
- Katika usiku wa nusu Sha'baan
- Katika usiku wa Israa' na Mi'raaj
- Katika usiku wa Qadr Ramadhaan
Mwaka ambao Mtume alifariki Jibriyl alikuja kumdarasisha Qur-aan mara ngapi?
- Mara 10
- Mara 5
- Mara 2
Inafaa kwa aliyehakikisha kuzama kwa jua kufungua hata kama hajasikia adhaana?
- Ndio, Sunnah ni kuharakisha kufungua
- Hapana, asubiri adhaana
- Akifungua hana swawm na lazima alipe siku nyingine
Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye ameangalia mapicha machafu?
- Hana swawm
- Swawm yake imeenda patupu siku hiyo na lazima alipe siku nyingine
- Swawm yake ni sahihi, lakini ina mapungufu na anapata madhambi
Je, imethibiti kwamba tendo jema la Ramadhaan malipo yake ni mara 70 ukilinganisha na miezi mingine?
- Haikuthibiti
- Imethibiti
- Analipwa thawabu 10 tu
Vipi swawm kwa kafiri aliyesilimu mchana wa Ramadhaan?
- Anapaswa kujizuia siku hiyo na ataanza kufunga siku ya kufuata
- Ataanza kufunga Ramadhaan ya mwaka unaofuata
- Alipa siku za Ramadhaan zilizompita
Ni vipi swawm ya mwanamke aliyehisi maumivu ya hedhi punde kidogo kabla ya jua kuzama?
- Ale na atafunga siku nyingine badala yake
- Atajizuia kula na kulipa siku nyingine
- Ataendelea na swawm yake midhali hajaona damu
Ni vipi hukumu ya swawm ya aliyempiga mtoto?
- Afungue hana swawm
- Swawm ni sahihi
- Swawm ina mapungufu
Anaruhusiwa ambaye ameswali na imamu Tarawiyh kusimama usiku kuswali tena?
- Ndio, ila tu asiswali Witr mara ya pili kama alishaswali msikitini
- Hapana, hiyo ni Bid'ah
- Ndio, pia aswali Witr mara ya pili kwani hiyo ni ziada ya kheri