Jipime maarifa yako kuhusu swawm
Chemsha Bongo ya Ramadhaan 05
15:00
Ni lini kuna matarajio makubwa zaidi ya kupata usiku wa Qadr?
- Tarehe 10 Ramadhaan
- Zile nyusiku za witiri khaswa usiku wa 27 Ramadhaan
- Tarehe 30 Ramadhaan
Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye kumeadhiniwa Fajr akiwa na chakula mdomoni?
- Amefungua na lazima afunge siku nyingine badala yake
- Aendelee kula ila afanye haraka kumaliza
- Ameze kilichomo tayari mdomoni mwake ila asichukue kingine na swawm yake ni sahihi
Je, inafaa kutegemea Hesabu juu ya kuanza na kumalizika mwezi wa Ramadhaan?
- Inafaa haina neno
- Inachukiza kufanya hivo kila mwaka
- Haifai, waislamu wanategemea kuangalia mwezi
Inafaa kujifunika shuka moja na mke mchana wa Ramadhaan?
- Haifai kabisa
- Inafaa haina neno
- Inafaa tu kama wanandoa wote hawakufunga
Ni yepi malipo ya mwenye kusimama usiku wa Qadr kwa imani na matarajio?
- Ni sawa na aliyehiji na Mtume
- Ataingia Peponi bila ya hesabu
- Atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia
Ni ipi hukumu ya muislamu asiyefunga Ramadhaan bila udhuru wowote?
- Ni kafiri
- Ni mtenda dhambi kubwa
- Ni mtenda dhambi ndogo
Ni upi usahihi wa Hadiyth inayosema kumi la kwanza la Ramadhaan ni la rehema, la pili ni la msahama na la tatu kuachwa huru na Moto?
- Swahiyh
- Dhaifu
- Ni maneno ya Swahabah
- Ni maneno ya wanazuoni
Nini imesuniwa kusema kwa mwenye kukutukana ilihali umefunga?
- Nawe mtukane kama yeye ndiye kakuanza
- Mwambie "Salaam!"
- Mwambie "Mimi nimefunga!"
Ni ipi hukumu ya mnyonyeshaji asiyeweza kufunga Ramadhaan?
- Ataacha huru mtumwa juu ya kila siku aliyokula
- Ni lazima afunge kwa hali yoyote
- Baba wa mtoto atamsaidia kufunga
- Kama anachelea nafsi yake na mtoto wake atalipa na kulisha masikini mmoja kwa kila siku aliyofungua
Je, inafaa kwa mwenye kukaa Itikaaf kutoka msikitini?
- Ndio, inafaa kwa hali yoyote
- Hapana, ila kama kuna dharurah
- Ndio, ila asifanye masaa mengi nje ya msikiti
Ni ipi hukumu ya swawm ya aliyetapika?
- Andelee na swawm yake kwani hakukusudia
- Afungue na badala yake afunge siku nyingine
- Huyo ni mgonjwa na lazima afungue
Ni lini unaanza muda wa Itikaaf?
- Fajr ya tarehe 1 Ramadhaan
- Fajr ya tarehe 27 Ramadhaan
- Baada ya swalah ya Fajr tarehe 21 Ramadhaan
Ni ipi kafara ya mfungaji aliyefanya tendo la ndoa na mkewe mchana wa Ramadhaan?
- Kulisha chakula masikini 10
- Kuacha huru mtumwa
- Kufunga siku 40 kwa mfululizo
Ni ipi hukumu ya mjamzito asiyeweza kufunga Ramadhaan?
- Kama anachelea nafsi yake na mtoto wake atalipa na kulisha masikini mmoja kwa kila siku aliyofungua
- Atafunga badala yake siku 60
- Atalisha masikini wawili kwa kila siku moja aliyokula
- Ni lazima afunge kwa hali yoyote
Ni lini unaisha muda wa Itikaaf?
- Aswr ya tarehe 15 Ramadhaan
- Dhuhr ya tarehe 27 Ramadhaan
- Kuzama kwa jua ile siku ya mwisho ya Ramadhaan
Ambaye hakufunga Ramadhaan anaweza kukaa Itikaaf?
- Hapana kabisa
- Anaweza na hakuna mahusiano kati ya hayo mawili
- Anaweza tu kama amefunga
Inafaa kuswali Rakah tatu za Witr kwa salamu moja?
- Hapana, haifai
- Inafaa tu kama amechoka sana
- Ndio, inafaa
Imesuniwa kusema nini baada ya swalah ya Witr?
- Alhamdulillaah wa swalaatu was-Salaam 'alaa Rasuulillaah
- Astaghfirullaah mara 3
- Subhaana Malikul qudduus mara 3, kisha Rabbul Malaaikati war-Ruuh mara 1
Je, mtu anaweza kukaa Itikaaf miezi mingine nje ya Ramadhaan?
- Ndio, anaweza
- I'tikaaf inakuwa mwezi wowote kwa aliyefunga tu
- Hapana, hawezi
Je, inafaa kufunga siku ya shaka kwa ajili ya kuchukua tahadhari?
- Haijuzu ila kwa aliyezowea kufunga hapo kabla
- Inajuzu na hakuna ubaya wowote
- Swawm ni ´ibaadah kubwa na hivyo inapendeza
Inafaa kwa mwenye udhuru wa kufunga (kama mwenye hedhi) kula hadharani mchana wa Ramadhaan?
- Hapana haifai, ale kwa kujificha
- Inafaa kwani yuko na udhuru wa kishari'ah
- Inafaa tu kula jua likishazama
Ni wapi mtu anatakiwa kukaa Itikaaf?
- Nyumbani
- Msikitini
- Kote tu ni sawa