Jipime maarifa yako kuhusu swawm

Chemsha Bongo ya Ramadhaan 02

15:00

Ni ipi hukumu ya swawm ya mfungaji anapodunga sindano?

  • Haifai na ni dhambi
  • Sindano aina zote zinafaa

Ni lini mwisho wa kula daku?

  • Jua linapochomoza
  • Saa kumi alfajiri

Bora kwa mwanamke kuswali Tarawiyh wapi?

  • Msikitini
  • Popote muhimu aswali

Ni ipi hukumu ya swawm ya mfungaji aliyekula kwa kusahau?

  • Inasihi lakini anapata dhambi
  • Ameze tu kwa sababu amesahau

Ni ipi hukumu ya swawm ya mgonjwa ambaye anang´ang´ania kufunga?

  • Haisihi kwa sababu anatakiwa kula
  • Haisihi kama anasafiri mji mmoja hadi mwingine

Ni ipi hukumu ya swawm ya mjamzito?

  • Inasihi
  • Inachukiza

Je, kutumia dawa ya kupaka ngozi inaharibu swawm?

  • Ndio, kwa kuwa dawa zinaweza kufyonzwa mwilini
  • Inategemea ikiwa mtu atahisi nguvu baada ya kupaka

Ni wakati gani bora kula daku katika nyakati hizi?

  • Katikati ya usiku
  • Wakati wowote midhali ni kabla ya adhaana

Ni ipi hukumu ya swawm ya mfungaji aliyetokwa na wadiy na madhiy?

  • Vyote viwili vinaharibu swawm
  • Vyote viwili haviharibu swawm

Ni Sunnah kufungua swawm kwa kitu gani unapokosa tende?

  • Asali
  • Maziwa
  • Maji

Mtume alifunga Ramadhaan ngapi kabla ya kufariki kwake?

  • 9
  • 2
  • 10

Ni vipi inawekwa nia ya kufunga Ramadhaan?

  • Kwa kutamka kila siku kabla ya saa sita usiku
  • Moyoni unaponuia kula daku au kufunga umetia nia
  • Kwa kutamkishwa na Shaykh msikitini

Ni ipi hukumu ya kufunga Ramadhaan kwa muislamu mwenye akili timamu na aliyebaleghe?

  • Sunnah iliyosisitizwa
  • Ni muhimu sana
  • Faradhi

Je, mtu anaweza kuoga maji baridi wakati wa mchana wa Ramadhaan?

  • Ndio
  • Hapana
  • Akoge, lakini kiasi kidogo tu

Je, mtoto ambaye hajabaleghe anawajibika kufunga Ramadhaan?

  • Ndio
  • Hapana, ila ni vyema kumpa mazoezi kama anaweza
  • Ni haramu kwake kufunga

Inafaa kwa wanandoa walio safarini kufanya tendo la ndoa wakati wa safari yao?

  • Hapana ni dhambi mchana wa Ramadhaan
  • Inafaa midhali ni wasafiri
  • Ni Sunnah

Ni ipi hukumu ya kula au kunywa kwa kusahau wakati wa Ramadhaan?

  • Hakufungua
  • Amefungua
  • Anapata dhambi

Je, ikiwa mtu atakusanya mate yake mwenyewe ameze, je, swawm yake itabatilika?

  • Ndio, yakiwa ni mengi
  • Ndio, kwa kuwa kitu chochote kinachopita koo kinaharibu swawm
  • Hapana

Je, inafaa kwa mume kumkumbatia mkewe wakati amefunga?

  • Hapana haifai
  • Ndio, inafaa muda wa kuwa hachelei kufanya jimaa
  • Inafaa tu baada ya kuzama jua

Ni ipi hukumu ya swawm ya ambaye hakuswali Tarawiyh?

  • Swawm yake si sahihi
  • Swawm yake ina mapungufu
  • Swawm yake inasihi, hakuna mafungamano ya hayo mawili

Je, mtu akikosa kula daku bado funga yake ni sahihi?

  • Hapana
  • Ndio
  • Kafanya dhambi

Nini maana ya swawm kwa mujibu wa Shari´ah?

  • Kuswali Tarawiyh
  • Kusoma sana Qur-aan
  • Kujiepusha na vifunguzi vyote