Jipime maarifa yako kuhusu ´Aqiydah sahihi
Chemsha Bongo ya ´Aqiydah sahihi 03
15:00
Imani ina tanzu (matawi) ngapi kwa mujibu wa Hadiyth mashuhuri ya Mtume?
- 100 na zaidi
- 70 na zaidi
- 50 na zaidi
Mtume aliwalingania washirikina katika Tawhiyd kwa miaka mingapi?
- 10
- 13
- 5
Ni vitabu vingapi ambavyo Allaah aliwateremshia Mitume Yake?
- 6
- 10
- 5
Ni ipi hukumu ya anayepinga adhabu ya ndani ya kaburi?
- Muumini mwenye imani pungufu
- Ni kafiri
- Ni suala lina makinzano kwa Ahl-us-Sunnah
Ni ipi haki ya Allaah kwa waja?
- Kumwabudu Yeye na kutomshirikisha na yeyote
- Kuwa na yakini kwamba yuko na amakuona kila mahali
- Kutambua kuwa Yeye ndiye mkubwa kuliko kila kitu
Je, inafaa kufanya ibaadah makaburini kama vile kusoma Qur-aan n.k.?
- Hapana, ni njia inayopelekea katika shirki
- Ndio, hapana ubaya wowote
- Inafaa kufanya 'ibaadah karibu na makaburi ya waja wema
Je, watu watafanyiwa hesabu na kulipwa kwa matendo yao baada ya kufufuliwa?
- Hapana
- Hakuna kitu kama hicho
- Ndio
Ni ipi haki ya viumbe kwa Allaah?
- Kutomwabudu asiyemshirikisha na chochote
- Allaah ana uwezo wa kusamehewa shirki
- Allaah si muweza wa kila kitu
Ni kipi sahihi katika haya?
- Allaah yuko kila mahali kwa dhati Yake
- Allaah yuko kila mahali kwa ujuzi Wake
- Allaah hayuko ndani ya ulimwengu wala nje ya ulimwengu
Ni ipi hukumu ya uchawi na mchawi?
- Muislamu mwenye imani pungufu
- Wanazuoni wametofautiana katika suala hilo
- Ni ukafiri na mchawi ni kafiri
Ni ipi hukumu ya anayechinja kwa ajili ya kujikurubisha kwa majini?
- Inafaa kama ni majini ya Kiislamu
- Ni muislamu, lakini Uislamu wake una mapungufu
- Ni kafiri, kwa.s amemfanyia 'ibaadah asiye Allaah
Ihsaan ina nguzo ngapi?
- 5
- 10
- 1
Ni ipi hukumu ya mwenye kumkufuru Mtume mmoja tu?
- Kafiri
- Muislamu muhimu ni kumwamini Muhammad
- Wanazuoni wametofautiana
Ni nani katika hawa watatu ambaye ametenda dhambi kubwa zaidi?
- Aliyefanya shirki
- Aliyemwingilia mama yake
- Aliyemwingilia dada yake
Ni ipi hukumu ya kwenda kwa mpiga ramli na kuhani?
- Ni dhambi ya kawaida
- Ni sawa na uzinzi
- Ni kufuru
Je, inafaa kutufu mahali popote zaidi ya Kabah?
- Ndio
- Hapana, kutufu kunakuwa kwenye Ka´bah pekee
- Kutufu kunaweza kufanywa pia kwenye kaburi la walii
Ni ipi ngazi ya pili katika ngazi za Uislamu?
- Imani
- Uislamu
- Ihsaan
Ni ipi hukumu ya anayepinga kufufuliwa?
- Muumini mwenye imani pungufu
- Muislamu mtenda dhambi kubwa
- Kafiri
Je, inafaa kutafuta baraka kutoka kwa kiumbe?
- Ndio, kama ni mtu mwema
- Hapana, isipokuwa kama ni kiumbe ambacho Allaah amekifanya kuwa na baraka kama maji ya zamzam
- Mambo ya baraka hakuna kabisa
Kuna aina ngapi za kufuru na ni zipi?
- 5; kubwa, ndogo, iliyojificha, iliyodhahiri na inayotambulika
- 1; kubwa tu
- 2; kubwa na ndogo
Je, inafaa kumwomba maiti akuombee dua au akusaidie jambo?
- Ndio, hapana vibaya kwani anasikia
- Hapana, hiyo ni shirki
- Inafaa kumwomba maiti kama ni walii peke yake
Ni ipi shirki ya kwanza kujitokeza ardhini?
- Uchawi
- Kuabudia waja wema
- Kuabudia mizimu